Saturday, May 11, 2013

Bomu lililolipuka Arusha limetengenezwa kienyeji - Mstaafu JW

ad300
Advertisement
Taarifa kutoka kwa mmoja wa maofisa wastaafu wa jeshi la wananchi Tanzania zinasema tukio la mlipuko wa bomu lililotokea hivi karibuni mkoani Arusha, limetengenezwa kienyeji.

Bomu hilo lilirushwa na kuua watu watatu na kujeruhi wengine zaidi ya 60 kwenye Kanisa Katoliki la Mtakatifu Joseph mtume eneo la Olasiti mkoani humo jumapili ya Mei 5 mwaka huu ambapo mwakilishi wa Mkuu wa kanisa hilo katoliki alihudhuria ibada ya siku hiyo ili kuweka wakfu parokia hiyo mpya.

Wakati taarifa hizo zinatoka, mazishi ya watu waliopoteza maisha katika tukio hilo, Regina Kurusei (45), James Gabriel (16) na Patricia Joachim (9) yamefanyika kanisani Olasiti, Arusha na Waziri Mkuu, Mheshimiwa Mizengo Peter Pinda alihudhuria.

Ofisa huyo mstaafu wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ), ambaye jina lake limehifadhiwa, alisema kuwa kwa ujuzi na uzoefu wake wa masuala hayo, bomu hilo si la kiwandani akisema msingi wa imani yake ni jinsi vyuma vilivyotawanyika na kuumiza watu zaidi ya 20.

Kwa mujibu wa taarifa kutoka gazeti mojawapo nchini zinasema ofisa huyo ameeleza kuwa kwa uzoefu wake na masuala ya milipuko wakati akiwa jeshini, ni wazi kuwa bomu hilo siyo la kiwandani bali limetengenezwa kienyeji kabisa.

Mstaafu huyo alieleza kuwa mabomu mengi zaidi ya kienyeji hutengenezwa kwa kutumia bakuli za chuma, zikiwekewa baruti ndani na kufungwa kwa waya.

“Hawa jamaa huweka vipande kama 36 vya baruti na hufungiwa ndani ya bakuli kwa kubanwa sana ili kuvipa joto na bomu likitua, husababisha madhara makubwa,” alisema ofisa huyo ambaye alishiriki Vita ya Uganda mwaka 1978 hadi 1979.

Aidha Mstaafu huyo alisema mabomu ya aina hiyo yametumika kwenye mashambulizi ya kigaidi katika nchi mbalimbali duniani kama Lebanon, Vietnam, Libya, Ireland Kaskazini, Syria, Afghanistan, Iraq, Chechnya na India.
Share This
Previous Post
Next Post

Pellentesque vitae lectus in mauris sollicitudin ornare sit amet eget ligula. Donec pharetra, arcu eu consectetur semper, est nulla sodales risus, vel efficitur orci justo quis tellus. Phasellus sit amet est pharetra

0 comments: