Advertisement |
Tukio hilo lilitokea juzi saa 2 usiku Jumapili
iliyopita maeneo ya Utemini ambapo alivamiwa na mtu huyo ambao mbali na
kumjeruhi kwa mapanga, pia alimpiga ngumi na mateke na kumjeruhi katika
jicho lake la kushoto.
Silla amelazwa katika Hospitali ya Mkoa wa Singida
ambapo alifikishwa na kijana mmoja (jina halikumbuki) ambaye alimkuta
akiwa hajitambui.
Hata hivyo, Kamanda wa Polisi mkoani hapa, Geofrey
Kamwela alipoulizwa kuhusu suala hilo alisema kuwa hana taarifa yoyote
na kuahidi kuwa atafuatilia tukio hilo.
Silla ni mwakilishi wa gazeti hili mkoani humo na huandika zaidi Makala za kijamii na kiutamaduni.
Tangu afikishwe katika hospitali hiyo, watu
mbalimbali walikwenda kumjulia hali akiwamo Mkuu wa Mkoa wa Singida, Dk
Parseko Kone.
Akisimulia mkasa huo akiwa hospitalini, Silla
alisema, nilikuwa nikirejea nyumbani muda ya jioni nilipofika maeneo ya
Utemini simu yake ya kiganjani ikaita na kulazimika kuzungumza ghafla
akatokea kijana ambaye alikuwa amejifunika shuka la kimasai na kuanza
kumfuata.
“Nilipogundua yule kijana ananifuata kwa kasi
nikaongeza mwendo lakini kila nilipojaribu kumkwepa alizidi kunifuata
mpaka nilipofika karibu na uzio wa nyumba moja akanikaribia na kuanza
kunivamia kisha kunibamiza katika geti la nyumba hiyo.”
Alisema baada ya kufanikiwa kunidhibiti akaanza
kunicharanga na mapanga huku akidai nimpatie pesa, nikamwambia sina pesa
lakini cha kushangaza akasema wewe huwa una hela.
“Alinishangaza sana, inaonekana kama ananijua,
lakini kila nilipokuwa namkaribia ili nimjue vizuri alikuwa anazidi
kunisukuma nisimgundue.”
Kwa mujibu wa Silla, mtu huyo alimnyang’anya simu
pamoja na mfuko uliokuwa na vifaa vidogo ambavyo alitoka kununua
yakiwamo mafuta. Chanzo 'Mwananchi Paper'
0 comments: