Tuesday, April 16, 2013

Mlipuko wa bomu waua, wajeruhi mbio za Marathon Marekani

ad300
Advertisement
WAKATI watu wawili wakifariki dunia na wengine 23 wakijeruhiwa vibaya katika milipuko miwili ya mabamu wakati wa mashindano ya mbio za marathon nchini Marekani, Rais Barack Obama amesema kwamba wahusika watajulikana.

Akizungumza na waandishi wa habari , Obama alisema kwamba amezungumza na viongozi wa vikosi mbalimbali vya upelelezi nchini humo pamoja na FBI na kumwakikishia kupata taarifa kamili ya watuhumiwa hao.

Watuhumiwa wa tukio hilo wanadaiwa kuwa ni magaidi waliokuwa na lengo la kuwa watu wengine wakati wa mashindano hayo ingawa haikujulikana maramoja kuwa ni magaidi kutoka nchi gani.

"Nimezungumza na vikosi vya Ulinzi na Usalama wa Marekani pamoja na  kikosi cha Upelelezi cha FBI na tayari wamesha anza kazi ya upelelezi wa tukio hilo, nina ahidi kwamba wahusika watapatikana na sababu iliyofanya walipue mabomu hayo pia itajulikana"alisema Obama.

Akizungumza kwa huzuni mkubwa huku akikataa kujibu maswali ya waandishi habari, Obama alisema kwamba tukio hilo haliwezi kuvumiliwa na kwamba hata siku moja watuhumiwa hao hawawezi kuachwa watoke nje ya mipaka ya Marekani kabla ya kukamatwa na kwamba ukaguzi umeanza mara moja sehemu zote zenye msongamano, njia zote za usafiri pamoja na hoteli zote nchini marekani.


Baadhi ya waokoaji wakifanya jukumu lao baada ya mlipuko wa mabomu kutokea jijini Boston nchini Marekani kwenye mbio za Marathon. Inasemekana moja ya bomu lilitegwa karibu na msitari wa kumaliza mbio.
Share This
Previous Post
Next Post

Pellentesque vitae lectus in mauris sollicitudin ornare sit amet eget ligula. Donec pharetra, arcu eu consectetur semper, est nulla sodales risus, vel efficitur orci justo quis tellus. Phasellus sit amet est pharetra

0 comments: