Friday, April 13, 2018

Werrason kutikisa Escape One Jumamosi hii

ad300
Advertisement

MWANAMUZIKI wa dansi kutoka nchini Congo, Werrason Ngiuma anatarajia kufanya tamasha la muziki Jumamosi hii Aprili 14, katika ukumbi wa Escape one Mikocheni, Dar es Salaam.

Akizungumza jijini Dar es Salaam, Meneja wa msanii huyo, Legos Vip, amesema ameamua kumleta mwanamuziki huyo kwa lengo la kuleta ushindani kwenye soko la muziki wa dansi Tanzania.

Amesema msanii Werrason ni muimbaji mahiri ambaye anaimba nyimbo zenye jumbe mbalimbali katika maisha ya binadamu.

“Nimeona ukubwa wake kwenye tasnia ya muziki wa dansi ndio maana tukamleta kwaajili ya kuburudisha watanzania wote ambao watakaoudhuria, kumleta msanii kubwa si jambo dogo.

“Si Mkoa wa Dar es Salaam peke yake bali ataenda hadi  Mwanza kwa ajili ya kuwapa burudani wakazi wa mkoa huo ambayo itafanyika  uwanja wa CCM Kirumba,” amesema Legos.

Ameongeza kuwa Werrason hatopanda jukwaani peke yake bali atakuwa na msanii wa muziki wa dansi  Christian Bella kwaajili ya kutoa  burudani kwa Watanzania.

Imeandikwa Amina Kasheba

Share This
Previous Post
Next Post

Pellentesque vitae lectus in mauris sollicitudin ornare sit amet eget ligula. Donec pharetra, arcu eu consectetur semper, est nulla sodales risus, vel efficitur orci justo quis tellus. Phasellus sit amet est pharetra

0 comments: