Friday, April 13, 2018

Super Star Bongo Movie waandaa tamasha la maana Iringa

ad300
Advertisement
WASANII wa bongo movie wameandaa tamasha 'concert' waliyoipa jina la ‘AMKA KIJANA NAFASI NI YAKO’ ambalo linatarajiwa kufanyika Aprili 14 hadi 18, mwaka huu, mkoani Iringa.

Wasanii watakao shiriki katika Concert hiyo ni Jackline Wolper, Irene Uwoya, Shamsa Ford, Aunty Ezikiel, Single Mtambalike, Wellu Sengo, Husna Sajenti, Jacob Steven(JB) na Steve Nyerere ambaye ndiye Mwenyekiti wa safari hiyo.

Steve Nyerere amesema lengo la Concert hiyo ni kuwaelimisha vijana wote ambao wamekata tamaa ya maisha na wale ambao wanatumia dawa za kulevya kwa kudhani ndio suluhu la tatizo.

Amesema wanatoa elimu kwa vijana ambao wanavipaji mbalimbali na wamevikalia chini bila hata kuvifanyia kazi yoyote kwa kudhani maisha ni magumu.

“Nia yetu ni kutoa elimu kwa vijana mbalimbali wa mikoa tofouti ambao wamekata tamaa ya maisha kwani vijana wengi wameharibika na dawa za kulevya na wengine wanakimbilia uko wakidhani ndio suluhu la tatizo.

“Concert hii itakuwa endelevu kwa mikoa yote ya Tanzania kwaajili ya kutoa elimu na kuwafunza vijana namna  kutumia fursa wasanii wa filamu tumeona tatizo hili  ndomaana  tumeamua kufanya kitu cha namna hii,” amesema Nyerere.

Amesema wasanii kwa ujumla wanaushukuru uongozi wa serikali awamu ya tano chini ya Rais Dk. John Magufuli, kwa kuhakikisha nchi inakuwa katika hali nzuri na kutokomeza mambo yote mabovu ambayo yalikuwa yanaliharibu Taifa.

Baada ya kumalizana na mkoa wa Iringa Nyerere Concert inatarajia kwenda mikoa ya Mbeya na Dodoma.

Imeandikwa na Amina Kasheba
Share This
Previous Post
Next Post

Pellentesque vitae lectus in mauris sollicitudin ornare sit amet eget ligula. Donec pharetra, arcu eu consectetur semper, est nulla sodales risus, vel efficitur orci justo quis tellus. Phasellus sit amet est pharetra

0 comments: