Advertisement |
NYOTA wa
muziki wa Bongo Fleva, Bernard Poul ‘Ben
Pol’ ametoa wimbo wake mpya uitwao ‘Napenda nipate lau nafasi’ ambao umekuwa
gumzo kutokana na staili aliimba.
Habari hii imeandikwa na Mwanaheri Masoud
Wimbo huo,
kwa mara ya kwanza uliimbwa na mwanamuziki Marijani Rashid, akiwa na bendi ya Kilwa
Jazz na kufanya vizuri zaidi katika stesheni mbalimbali za redio na televisheni
nchini.
Ben Pol
ambaye anatamba na nyimbo mbalimbali zikiwemo ‘Sophia’, ‘Natuliza bolli’ , ‘Jikubali’
na nyingine nyingi ambazo zinafanya vizuri kwenye vituo mbalimbali vya
televisheni na redio.
Ben Pol kwa
kushirikiana na msanii mwenzake Wyse wameamua kuurudia wimbo huo kutokana na mapenzi
na waimbaji wa bendi ya Kilwa Jazz.
“Mara nyingi
muziki wa bendi unavutia na unaujumbe mzuri, wengi waliotangulia kufanya muziki
huo walifanya vizuri hivyo nimevutiwa na wimbo wa Jazz Band Napenda lau nipate
nafasi kwa sababu ni nyimbo ambayo nikipenda sana kuisikiliza hapo
nyuma,” amesema Ben Pol.
Ben Pol amesema
marehemu Marijani na bendi zingine ikiwemo Sikinde, Moro Jazz,Tanka Talamasi na
Tabora Jazz ni miongoni mwa bendi ambazo zinamfanya atamani kufanya muziki
mzuri na pia kujifunza zaidi kupitia nyimbo zao .
Amesema
anayefanya kazi mzuri siku zote hukumbukwa kwa jitihada na uwezo wake hivyo
nyimbo hizo zitaendelea kuwa mfano wa kuigwa na wengi ambao wanapenda kujifunza
au kufanya muziki wa aina hiyo.
Kufuatia
uamuzi wa Ben Pol kuurudia wimbo huo huku akiuongezea vionjo, wapenzi wa muziki
huo nchini wamepongeza kazi hiyo huku wakisema ameutendea haki.
Habari hii imeandikwa na Mwanaheri Masoud
0 comments: