Advertisement |
Jumuiya ya Maendeleo ya Serikali ya Nchi za Afrika Mashariki IGAD
kwa mara nyingine imeanzisha mazungumzo ya amani kuhusu Sudan Kusini jana huko Addis
Ababa, mji mkuu wa Ethiopia, ambayo yametishia kuchukua hatua za
kuadhibu pande mbalimbali zinazopambana.
Mkutano huo unaoitwa Kipindi cha pili cha Baraza la ngazi ya juu la
ustawi umefanyika baada ya kusainiwa kwa Makubaliano ya kusitisha
mapambano Desemba 24 mwaka 2017, ambayo yalivunjika saa chache
baada ya kuanza utekelezaji wake.
Mjumbe maalumu wa IGAD kwenye suala la Sudan Kusini, Ismael
Wais amezitaka pande mbili zinazopambana zisitishe mapambano ili kuweka
na kuimarisha mafanikio, uaminifu na imani zilizoanzishwa na
Makubaliano ya kusitisha mapambano.
Amesema Umoja wa Afrika, IGAD, Umoja
wa Mataifa pamoja na jumuiya ya kimataifa zimetoa taarifa kali za
kulaani ukiukwaji wa makubaliano hayo.
0 comments: