Advertisement |
Ajali ya gari iliyotokea usiku wa kuamkia leo (Septemba 6), eneo la Ubena Zomozi mkoani Pwani imekatisha uhai wa viongozi wanne wa Chama cha Wananchi (CUF).
Viongozi hao waliofariki kutokana na gari lao kugongana na Lori ni wale wanaomuunga mkono Mwenyekiti wa chama hicho anayetambulika na Msajili wa Vyama, Prof. Ibrahim Lipumba.
Taarifa zinasema walikuwa kwenye msafara uliokuwa ukitoka Dodoma kwenye kushuhudia wabunge saba wa CUF wakila kiapo katika bunge la Tanzania baada ya kuteuliwa hivi karibuni.
Mkurugenzi wa Habari wa CUF, Abdallah Kambaya, alithibitisha tukio hilo na kusema viongozi waliofariki ni kutoka Wilaya ya Muheza, Tanga ambapo miongoni mwao alikuwepo Mgombea Udiwani wa Muheza Mjini, aliyefahamika kwa jina moja la Uledi.
Idadi ya majeruhi kwenye ajali hiyo bado haijajulikana.
Wapumzike kwa Amani!
0 comments: