Monday, August 14, 2017

Waziri Ndalichako ateta na wanafunzi Mkuranga

ad300
Advertisement
Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Profesa Joyce Ndalichako amewataka wanafunzi wa shule ya Sekondari Mwinyi na ile ya Nasibugani kuhakikisha wanasoma kwa bidii, na kuacha kujiingiza kwenye vikundi au mambo ambayo hayana tija kwa maendeleo ya Taifa.

 Waziri Ndalichako ameyasema hayo leo 14/8/2017, alipofanya ziara wilayani Mkuranga mkoani Pwani kwa lengo la kukagua ujenzi unaoendelea wa vyumba vya madarasa, mabweni na matundu ya vyoo katika shule hizo ambao unatekelezwa na  programu ya Lipa kulingana na matokeo.

Profesa Ndalichako amesema jitihada zinazofanywa na Rais John Magufuli za kuhakikisha Elimu bora inatolewa kwa wanafunzi zinapaswa kuungwa mkono kwa kuhakikisha kila mmoja anatimiza wajibu wake ipasavyo ikiwa ni pamoja na wanafunzi kufaulu vizuri.

Amesisitiza kuwa Serikali haihitaji kuona wanafunzi wanafeli bali  inataka kuona wanafunzi wanafaulu vizuri mitihani yao ya taifa, hivyo  kuwasihi walimu kutimiza majukumu yao kwa kuzingatia weledi.
Share This
Previous Post
Next Post

Pellentesque vitae lectus in mauris sollicitudin ornare sit amet eget ligula. Donec pharetra, arcu eu consectetur semper, est nulla sodales risus, vel efficitur orci justo quis tellus. Phasellus sit amet est pharetra

0 comments: