Tuesday, August 15, 2017

Pyongyang katika hatua za mwisho kuikabili Marekani

ad300
Advertisement
Vyombo vya habari nchini Korea Kaskazini vimeripoti kuwa watu zaidi ya milioni 3 wa kujitolea wametangaza utayari wao kwa ajili ya kupambana kwenye vita dhidi ya Marekani.

Gazeti la Rodong Sinmun la nchi hiyo, limeandika kwenye taarifa yake kuwa watu hao wamejiweka tayari kwa ajili ya kujitolea kupambana na Marekani iwapo nchi hiyo itaanzisha vita dhidi ya Korea Kaskazini.

Kwa mujibu wa habari hiyo, kikosi hicho cha kujitolea kinaundwa na raia wa kawaida, wafanyakazi wa umma na taasisi binafsi, askari waliostaafu na wanafunzi wa vyuo vya elimu ya juu.

Hatua hiyo imekuja baada ya Rais Donald Trump kutoa vitisho ambavyo havijawahi kushuhudiwa dhidi ya Korea Kaskazini katika siku chache zilizopita.

Kutokana na hali hiyo, Pyongyang nayo ilitishia kukamilisha mpango wa kuishambulia kwa makombora kambi za kijeshi za Marekani zilizoko katika kisiwa cha Guam kabla ya mwisho wa mwezi huu.

Wachambuzi wa masuala ya kiusalama walisema imani yao ni kwamba mgogoro wa eneo la Korea umeongeza kasi kutokana na siasa za uhasama za Marekani na washirika wake dhidi ya Korea Kaskazini.

Wakati huo huo Waziri Mkuu wa Australia, Malcolm Turnbull alitangaza kuwa, ikiwa Korea Kaskazini itaishambulia Marekani, nchi yake itashirikiana na Washington dhidi ya Pyongyang.

Turnbull aliyasema hayo baada ya Korea Kaskazini kutangaza kuwa ina mpango wa kushambulia kwa kombora kisiwa cha Guam katika bahari ya Pacific ambacho kiko chini ya umiliki wa Marekani.

Uungaji mkono wa serikali ya Canberra kwa Marekani umetangazwa baada ya Rais Donald Trump wa Marekani kuitishia Korea Kaskazini kwamba itashuhudia moto ambao haujawahi kushuhudiwa duniani.
Share This
Previous Post
Next Post

Pellentesque vitae lectus in mauris sollicitudin ornare sit amet eget ligula. Donec pharetra, arcu eu consectetur semper, est nulla sodales risus, vel efficitur orci justo quis tellus. Phasellus sit amet est pharetra

0 comments: