Advertisement |
Waziri
wa Maliasili na Utalii, Profesa Jumanne Maghembe amewaagiza wadau wa miti
wanaotumia misumeno aina ya Ding dong kuacha mara moja kwa sababu haina ufanisi
na inapoteza kiasi kikubwa cha magogo.
Alisema
umefika wakati wakatumia misumeno ya kisasa ambayo inaufanisi mkubwa kwenye
upasuaji mbao na ni rafiki wa rasilimali za misitu ikilinganishwa na iliyokuwa
ikitumiwa awali.
Waziri
alitoa kauli hiyo mkoani Iringa, alipozuru shamba la miti la Sao Hill na
kuzungumza na wadau wa shamba hilo wakiwemo wenye viwanda vya kupasulia mbao.
Katika
mkutano wake na wadau hao Aidha, Waziri Maghembe alitangaza kupunguza bei
ya miti aina mikaratusi kuanzia mwaka huu
ambapo ada ya tozo za barabara imepunguzwa kutoka shilingi 35,000 hadi shilingi
17,800.
Alisema
ameamua kuchukua uamuzi huo mara baada ya kupokea maombi ya wadau wengi kuhusu
kupunguza bei ya tozo hizo.
Waziri
huyo pia alitumia fursa hiyo kupiga marufuku wanavijiji waojaribu kumega eneo
la msitu kwa ajili ya shughuli nyingine kwamba eneo la msitu halimegwi kwa
kigezo chochote.
‘’Hakuna
kipande chochote cha ardhi katika shamba hili kitakachochukuliwa kwa ajili ya
shughuli nje ya hii inayofanyika kwa sasa,’’ alisisitiza Waziri Maghembe.
Aidha
alisisitiza vijiji vya jirani la shamba hilo viendelee kupata fedha za mgawo wa
miti ili wazitumie kwa shughuli nyingine za maendeleo.
Kwa
upande wa Mkuu wa Mkoa wa Iringa, Amina Masenza, alisema kuwa utaratibu
uliotumika mwaka huu wa ugawaji wa malighafi umekuwa mwarobaini wa kupunguza
malalamiko kwa wadau ukilinganisha na miaka iliyopita.
Aidha,
aliawapongeza wafanyabiashara na wadau wa shamba hilo kwa kulipa kodi stahiki
za Serikali.
Kutokana
na uamuzi huo wa serikali, wadau hao wa shamba la Sao Hill walisema
wameridhishwa na utendaji wa Waziri wa Maliasili na Utalii, Profesa Jumanne
Maghembe kwenye suala la ugawaji wa malighafi ya miti.
0 comments: