Advertisement |
Klabu ya Barcelona yenye makao yake Camp Nou, nchini Hispania imekamilisha usajili wa kinda mshambualiji wa Borrusia Dortmund, Ousmane Dembele, kwa uhamisho wa kitita cha pauni milioni 135.5.
Mchezaji
huyo wa Ufaransa mwenye umri wa miaka 20 ametia saini mkataba wa
miaka mitano katika uwanja wa nyumbani wa Barca Nou Camp akiwa na rais wa klabu hiyo Josep
Maria Bartomeu.
Mkataba huo ni wa pili kwa thamani baada ya ule wa hivi karibuni ya Neymar kuelekea PSG uliogharimu kitita cha pauni milioni 200.
Akizungumza kwenye mahojiano yake na TV Barcelona, Dembele alisema anafurahia sana kujiunga na Barcelona.
"Ilikuwa ndoto yangu tangu nikiwa mdogo kuichezea Barca na sasa imetimia," alisema.
Aliongeza kwa kusema kuwa kwake yeye Barca ndio klabu bora duniani yenye wachezaji bora duniani.
Mara ya mwisho kwa Dembele kuichezea Dortmund ni kwenye kombe la Supercup Agosti 5, mwaka huu.
Awali klabu
hiyo ya Bundesliga ilikataa ombi la Barca mapema Agosti, mwaka huu huku
mchezaji huyo akiwa amepewa marufuku kwa kukosa mazoezi.
Dembele anakwenda Barca kuziba pengo la Neymar, ataweza? Tusubiri tuone
0 comments: