Advertisement |
Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS) umeanza
kukusanyaji maduhuli kwa njia ya kielektroniki kufuatia marekebisho ya
sheria ya fedha ya mwaka 2017.
Pamoja
na sheria hiyo, pia umefanya hivyo kutekeleza maagizo ya serikali ya
awamu ya tano kupitia kwa Rais Dk. John Magufuli aliyezitaka taasisi za
umma kujiunga na mfumo wa kisasa wa ukusanyaji maduhuli.
Mfumo
huo uliotajwa na serikali ni ule uliosanifiwa na Wizara ya Fedha na
Mipango ambao unafahamika kwa jina la kitaalamu kama Government
electronic Payment Gateaway (GEPG).
Akizungumzia
mfumo huo jijini Dar es Salaam, Mhasibu Mkuu wa TFS, Peter
Mwakosya, alisema mashamba yote na ofisi za mameneja (DFM's) wa Taasisi
hiyo zimeunganishwa katika mfumo huo.
Pater
alisema kutokana na mazingira ya vizuizi (checkpoints) kutokidhi
mahitaji ya mfumo huo hususan kushindwa kuhifadhi vitendea kazi, wakala
unaendelea kuunganisha vizuizi vyote kwenye mfumo kwa kutumia vifaa
maalumu vinavyoitwa POS.
"Kutokana na changamoto zilizoko kwenye vizuia vyetu, hasa kwenye kukosa miundombinu ya kutunza vifaa muhimu kwa mfumo huu kama kompyuta kwa sasa vizuia vyote tunaviunganisha kwa POS, " alisema.
Alifafanua
kuwa vifaa hivyo vitatumika kukusanya maduhuli na kuhakiki uhalali wa
nyaraka zinazokaguliwa katika vituo vyote vya ukaguzi wa mazao ya misitu
na nyuki kwa kipindi hiki ambacho vizuizi vinaunganishwa kwenye mfumo
wa moja kwa moja.
Pamoja
na hayo, alisisitiza maduhuli yote yatakayokusanywa kwenye vizuizi
yawasilishwe mapema katika Ofisi za Mameneja wa Misitu wa wilaya ili
yaingizwe kwenye mfumo.
"Tuwakumbusha
wateja wote wa Mazao ya Misitu na nyuki pia kuzingatia kwamba
wanatakiwa kupata hati za madai (Bill) katika mfumo kabla ya kwenda
kufanya Malipo, ni muhimu sana," alisema.
Aliongeza
pia kwamba wateja hao wa bidhaa za Misitu na nyuki waliokuwa wakitumia
stakabadhi zingine kabla ya mfumo huo (ERV), hawataendelea kuzitumia
katika vituo vilivyounganishwa na mfumo wa sasa.
Miezi
michache iliyopita, Rais Dk. Magufuli aliagiza taasisi za umma kutumia
mifumo ya kisasa kukusanya fedha za serikali ili zisipotee mikononi mwa
wajanja wachache agizo lililotekelezwa na TFS kama moja ya taasisi
hizo.
0 comments: