Wednesday, August 23, 2017

Panya wavuruga kikao cha baraza la mawaziri

ad300
Advertisement
Kikao cha kwanza cha baraza la mawaziri wa Nigeria ambacho kilikuwa kifanyike kwa mara ya kwanza baada ya Rais Muhammadu Buhari kutoka likizo ya matibabu ya miezi mitatu nchini Uingereza kimeahirishwa.
 
Msemaji wa Buhari, Femi Adesina ametoa habari za kuahirishwa kikao hicho cha baraza la mawaziri bila kutoa maelezo zaidi   hukuRais Buhari mwenyewe akiwaandikia barua wabunge wa nchi hiyo akiwajulisha kuwa amerejea na ameanza kazi rasmi  .

Taarifa zaidi kutoka nchini humo kuhusu kuahirishwa kwa kikao hicho zimesema Rais Buhari anasubiri kukamilika kwa ukarabati wa ofisi yake ndipo akutane na chombo hicho kikuu cha maamuzi na utendaji serikalini.

Hayo yanajiri siku moja baada ya tangazo lililoeleza kuwa Buhari atafanyia kazi nyumbani kwake kwa wiki tatu baada ya kurudi nchini humo na kukuta ofisi yake iliyoko kwenye ikulu ya nchi hiyo ikiwa imeharibiwa na panya.

Msemaji wa rais alithibitisha uharibifu huo na kusema kwamba ofisi ya Buhari inakarabatiwa kwa wiki tatu baada ya panya kuharibu samani na mfumo wa kiyoyozi ndani ya ofisi hiyo.

Aliongeza kuwa licha ya Rais Buhari kulazimika kufanya kazi nje ya ofisi yake kutokana na hali ya ofisi hiyo kwa sasa, hatua ya kutumia nyumba yake kama ofisi haitaathiri kivyovyote utendaji wake wa kazi.

Wakati akipata matibabu Uingereza, Buhari alikabidhi uongozi kwa makamu wake, Yemi Osinbajo ambapo alirejea Nigeria Jumamosi ya wiki iliyopita.
Share This
Previous Post
Next Post

Pellentesque vitae lectus in mauris sollicitudin ornare sit amet eget ligula. Donec pharetra, arcu eu consectetur semper, est nulla sodales risus, vel efficitur orci justo quis tellus. Phasellus sit amet est pharetra

0 comments: