Tuesday, August 29, 2017

Mbunge awajulia hali majeruhi, wafiwa ajali ya Lori Singida

ad300
Advertisement

Mbunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Singida, Aysharose Mattembe, (mwenye kilemba cha njano pichani), amewatembele na kuwajulia hali majeruhi wa ajali ya lori lililokuwa limewabeba wafanyabiashara kutoka mnadani, kwenye Kijiji cha Kijota, Singida Vijijini.

Katika ziara hiyo kwenye hospitali ya rufani ya mkoa wa Singida ambako majeruhi hao wanaendelea na matibabu, aliwatakia kheri ili wapate nafuu ya haraka na kurudi majumbani mwao kuendelea na shughuli za ujenzi wa taifa.

Baada ya kutoka hospitalini hapo, mbunge huyo aliwatembelea wafiwa waliopoteza ndugu na jamaa kwenye ajali hiyo na kuwapa mkono wa pole huku akiwataka kuwa na moyo wa ujasiri wakimshukuru Mwenyezi Mungu kwa kila jambo kwa kuwa yeye ndiye mwamuzi wa yote. 

Katika ajali hiyo iliyotokea hivi karibuni mkoani Singida, watu wanane walifariki dunia na wengine 20 kujeruhiwa.

Share This
Previous Post
Next Post

Pellentesque vitae lectus in mauris sollicitudin ornare sit amet eget ligula. Donec pharetra, arcu eu consectetur semper, est nulla sodales risus, vel efficitur orci justo quis tellus. Phasellus sit amet est pharetra

0 comments: