Wednesday, August 23, 2017

Mahujaj wanusurika kifo Mecca

ad300
Advertisement
Mamia ya mahujaji wamenusurika kifo kufuatia ajali ya moto uliozuka katika jengo la ghorofa 15 mjini Mecca nchini Saudi Arabia.

Msemaji wa Idara ya Polisi wa Mecca, Naif Al Sharif alisema katika harakati za kuzima moto huo, jeshi hilo limefanikiwa kuwaokoa mahujaji 600 waliokuwa wamekwama katika jengo.

Alisema mahujaji hao walioko nchini humo kwa ajili ya hijja, wanatoka mataifa ya Yemen na Uturuki na kwamba hakuna mtu aliyefariki dunia katika tukio hilo la kushtusha.

Kwa upande wao polisi wa Saudia ilisema inaendelea na uchunguzi kubaini chanzo cha moto huo ambao ulianzia katika ghorofa ya nane kupitia mfumo wa kuingiza baridi ndani ya jengo hilo.

Siku chache zilizopita baadhi ya watu waliishutumu mamlaka ya Mecca kuwa dhaifu kwenye usalama wa mahajaji baada ya jengo jingine la mahujaji wa Nyumba ya Mwenyezi Mungu (al-Kaaba) mjini humo kuwaka moto.

Usimamizi mbovu wa viongozi wa Saudia katika kusimamia ibada ya Hijja umetajwa kuwa chanzo cha vifo vya mamia ya mahujaji kila mwaka.

Tukio baya zaidi kuwahi kurekodiwa kwenye vitabu vya historia ni lile la maafa ya Mina lililotokea miaka miwili iliyopita na kusababisha vifo vya zaidi ya Mahujaji 7,000.

Kwa mujibu wa takwimu zilizotolewa na viongozi wa Saudia, idadi ya mahujaji wa kigeni mjini Mecca ilipungua kwa asilimia 20 kwa mwaka jana ikilinganishwa na mwaka juzi hadi kufikia milioni moja na laki nane pekee.

Miaka mitano iliyopita, takwimu za Hijja katika mji huo mtakatifu wa Mecca zilirekodi mahujaji zaidi ya milioni tatu kwa mwaka.
Share This
Previous Post
Next Post

Pellentesque vitae lectus in mauris sollicitudin ornare sit amet eget ligula. Donec pharetra, arcu eu consectetur semper, est nulla sodales risus, vel efficitur orci justo quis tellus. Phasellus sit amet est pharetra

0 comments: