Friday, August 18, 2017

Lissu awashutumu Polisi, TISS

ad300
Advertisement
Mbunge wa Singida Mashariki na Mwanasheria Mkuu wa Chadema, Tundu Lissu amedai anafuatiliwa na watu anaowashuku kuwa ni Maafisa Usalama, katika kipindi cha wiki tatu mfululizo. Hata hivyo hajabainisha sababu ya kufuatiliwa kwake.

Lissu ameyaeleza hayo jijini Dar es Salaam wakati akizungumza na wanahabari na kuwanyooshea kidole Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini, IGP Simon Sirro pamoja na Mkuu wa Idara ya Usalama wa Taifa (TISS).

Alidai wakuu hao wanapaswa kuwaeleza wakubwa wao kuhusu maagizo yao kwa watumishi hao kupambana na wahalifu badala ya kutumia rasilimali za nchi kufuatilia raia wasio na hatia.

Lissu amedai kuwa, watumishi hao wanapaswa kutumia vema rasilimali za nchi kwa kupambana na wahalifu badala ya kuhangaika na wananchi wanaotimiza wajibu wao kikatiba katika kuwawajibisha baadhi ya viongozi wasiotimiza wajibu wao.

“Mkuu wa TISS au IGP wale vijana mliowatuma wiki tatu mfululizo kunifuata kila nilipo, niliowakaba Kanisani St. Peter, muwaambie wakubwa wawaelekeze watumishi wao kutumia muda na rasilimali za nchi kupambana na wahalifu na si kuhangaika na raia wanaotimiza wajibu wao kikatiba kuwawajibisha viongozi serikalini,” alisema.
Share This
Previous Post
Next Post

Pellentesque vitae lectus in mauris sollicitudin ornare sit amet eget ligula. Donec pharetra, arcu eu consectetur semper, est nulla sodales risus, vel efficitur orci justo quis tellus. Phasellus sit amet est pharetra

0 comments: