Friday, July 28, 2017

Wadau tushirikiane kutatua changamoto - Profesa Ngaruko

ad300
Advertisement
NA VINCENT MPEPO

Profesa Deus Ngaruko
Naibu Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu Huria cha Tanzania (Taaluma), Profesa Deus Ngaruko, amesema kuna umuhimu kwa wadau mbalimbali ikwemo serikali, waajiri na taasisi za elimu ya juu kushirikiana ili kupata majibu ya changamoto mbalimbali zinazoikabili jamii ya watanzania.

Amesema wajibu wa taasisi za elimu ya juu ni kufanya tafiti zitakazosaidia kupata majibu na tafsiri sahihi ya ajira akisisitiza kuwa ni muhimu kwa jamii kuwa na mawazo chanya kwa kazi halali zinazowaingizia wanaojiajiri vipato zaidi kuliko walioajiriwa katika sekta rasmi.

“Serikali inapaswa kutambua shughuli halali zinazofanywa na wahitimu wa vyuo vyetu kwa kuwa zinahusisha mawazo yao katika kuongeza ubora wa bidhaa na utafutaji wa masoo vitu ambavyo wamefundishwa vyuoni,” alisema Profesa Ngaruko.

Profesa huyo alisema akitolea mfano wa ajira ambazo zinafanywa na wahitimu ambao ni zao la taasisi za elimu ya juu nchini, kuwa bado ni tatizo la jamii kufahamu dhana ya ajira kwa kuwa taasisi na mamlaka husika hazijatambua mchango wake katika uchumi wa mtu mmoja mmoja na taifa.

“Kuna wahitimu wa vyuo vyetu hapa Tanzania wanafanya shughuli za ujasiriamali kama biashara ya saluni za kiume au za kike na wanapata kipato kizuri tofauti na walioajiriwa kwenye sekta ya umma,” alisema.

Profesa huyo alisema wao kama Chuo Kikuu Huria, kwa nafasi yao kutokana na  mfumo wao wa utoaji elimu kwa masafa kwa kutumia teknolojia za kisasa, wamefanikiwa kuwabadilisha vijana waliohitimu kidato cha sita na kuamua kujiendeleza na elimu huria, ambao wanajiajiri wakati wakiendelea na masomo.

Alisema kundi hilo linaweza kufanya shughuli zao binafsi kutokana na utaratibu uliowekwa na chuo, kwamba haumbani mwanafunzi kutumia muda wake wote chuoni lakini pia haumlei awe mzigo kwenye utumishi bali humwandaa awe na ufanisi utakaotoa mchango chanya kwa taifa kimaendeleo.

Naibu Mkuu huyo wa Chuo alitoa kauli hiyo kufuatia maagizo ya Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa, aliyovitaka vyuo vikuu nchini kuunga mkono juhudi za serikali kufikia uchumi wa kati na viwanda kwa kuandaa na kutoa wahitimu watakaosaidia katika sekta mbalimbali za uchumi wa nchi hususani kwenye viwanda.

Waziri Mkuu alisema hayo wakati akifungua maonesho ya 12 ya vyuo vikuu yanayofanyika katika viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es salaam na kuhudhuriwa na taasisi za elimu ya juu zaidi ya 80 za ndani na nje ya nchi.

Akihutubia kwenye uzinduzi huo, alisema wakati umefika amabapo vyuo vikuu vinatakiwa kuwa na mitaala ya kufundishia inayoendana na nia na mipango mikakati ya serikali ili kufikia adhma ya uchumi wa kati na viwanda.

“Wakati umefika kwa vyuo vya elimu ya juu na wanataaluma kufanya tafiti ili kupata majibu ya changamoto mbalimbali zinazokabili taifa ikiwemo ukosefu wa ajira”, alisema Majaliwa.

Pia alisema tasisi za elimu ya juu zina jukumu la kuandaa wahitimu watakaoweza kutatua changamoto ya ukosefu wa ajira kwa kujiari na kutoa msukumo kwenye sekta ya viwanda ili kukuza uchumi wa nchi.

Maonyesho hayo ya 12 ya taasisi za elimu ya juu ambayo Chuo Kikuu Huria cha Tanzania ni mmoja wa washiriki yanaratibiwa na Tume ya Vyuo Vikuu Tanzania (TCU).

Share This
Previous Post
Next Post

Pellentesque vitae lectus in mauris sollicitudin ornare sit amet eget ligula. Donec pharetra, arcu eu consectetur semper, est nulla sodales risus, vel efficitur orci justo quis tellus. Phasellus sit amet est pharetra

0 comments: