Monday, July 31, 2017

Tunaanzaje kuibeza Arsenal

ad300
Advertisement

Na ABDUL DUNIA

Ilikuwa saa 1:00 jioni katika moja ya kibandaumiza pale Buguruni. Nikiwa na babu yangu mzee Dunia nilikuwa nikishangilia ubingwa wa Arsenal mithili ya kuwa nilikuwa pale Highburry nchini England. Hakika ubingwa ule ulinifurahisha sana.

Tunaongozwa 2-0 katika mechi ya mwisho ya EPL dhidi ya Leicester City. Dakika chache kabla ya mechi kuisha nguvu za kile kikosi cha wachezaji 11 zinaonekana. Hakika ilikuwa The Dream Team. Hadi mechi ile inakwisha tunaongoza 4-2. Arsenal inabeba ubingwa kwa heshima ya hali ya juu. Unataka nini tena?

Kuna sababu nyingi za kuipenda Arsenal. Kuna kila sababu ya kuipenda Gunners. Unaachaje kuipenda Arsenal? Unaanzaje kuibeza Arsenal ambayo ina kila sababu ya kupendwa na kuheshimiwa? Ngoja nifungue hii barua b=niliyotumiwa na huyu shabiki wa Chelsea.

Watu wengi kipindi kile walikuwa wakishabikia Arsenal na Manchester United. Kuna anayebisha? Hivi wale vijana wanaoshabikia Chelsea walipata wapi ujasiri wa kufanya hivyo? Kipindi kile kijana huwezi kushabikia Chelsea.
Timu zilikuwa mbili tu. Arsenal na Manchester United kidogo Liverpool ila ilikuwa kwa wazee tu. Eti kijana wa sasa naye anaipenda Liverpool. Ushabiki gani huu?

Tunaanzaje kuibeza Arsenal? Kijana mwenye nguvu zake anapayuka mitaani na hata viwanjani bila ya kuona haibu. Anaweza kukuuliza kuwa 'Unashabikia Arsenal?, eti ndio maana unakonda. Shame on Them.

Jibu lake ni rahisi tu. Nashabikia Arsenal timu iliyotwaa ubingwa bila kufungwa, timu iliyoifunga Real Madrid iliyotimia katika Ligi ya Mabingwa Ulaya. Madrid ikiwa na Zidane, Guti, R. Carlos, Ronaldo Luis Nazario De Lima ilikubali kichapo palepale Emirates.

Unaanzaje kukataa kuishabikia Arsenal ambayo ilikuwa na viungo hatari duniani kama Patrick Viera, Petit, Roberto Pires, Alexander Helb na wengine. Mnamkumbuka yule Davor Suker, mtu hatari kutokea duniani? Zidane na uwezo wake wote lakini anamkumbuka 1998. Hakika Zidane alikubali alichokifanya binaadamu huyu.

Lee Dixon, Keown bado hawatoshi kuwatia haibu ya kuisema vibaya Arsenal? Heri mashabiki wa Manchester, kuliko wale wa Chelsea. Arsenal ile imesahaulika kweli hadi mnapayuka. Tumemsahau Thiery Henry alipokuwa akiwatambaza akina Stam? Viera akiwafanya vibaya akina Makelele na Roy Keane. Kipa Seaman, kipa Lehman unataka nini tena zaidi ya kuipenda Arsenal?

Unaanzaje kuibeza Arsenal wakati wewe umeanza kuishabiki Chelsea baada ya kuihama Arsenal baada ya kufungwa fainali ya UEFA dhidi ya Barcelona? Umeanza kuishabikia Chelsea baada ya kuihama United? Chelsea haijafikia makali hadi kufikia hatua ya kuibeza Arsenal.

Chelsea hii ambayo inashindana na Aston Villa kwa vikombe tunaanzaje kuibeza Arsenal? Tuambiane tu bila ya kupepesa macho. Hatuwezi kuibeza Arsenal. Tunaipenda Arsenal hatumpendi Wenger. Lazima tuelewe tunachokiandika na kusema. Arsenal is still Arsenal and Wenger is Wenger.

Haya nyie wa Liverpool tangu Ligi Kuu ya England inabadilishwa jina na mfumo 1992, mmeshawahi kutwaa ubingwa wa ligi? Tukiacha ile ya Instambul tuonyesheni kabati lenu la vikombe kama hakuna mende na chawa. Samahani ila acha iwe hivyo tu. Haina jinsi.

Ghafla nimelikumbuka lile bao murua la fundi Denis Berkamp dhidi ya Newcastle United miaka 14 iliyopita, ilikuwa mechi ya Ligi Kuu England (EPL). Alipoulizwa kuwa alifungaje alishindwa kujibu zaidi ya kusema kuwa ni mipango ya Mungu. Hakika lilikuwa bonge la Bao.

Pale ndipo nilipoanza kuipenda Arsenal. Nakumbuka mwaka ule nilikuwa nakwenda katika kibanda umiza nikiwa nimeshikwa mkono na babu yangu. Babu anashangilia Manchester alafu mjukuu anashangilia Arsenal. What a football? This is fair play Game.

Sikuwahi kurithishwa timu ya kuishangilia kama wengine wanavyorithishwa. Kijana uliyetimia unaanzaje kuishangilia Chelsea alafu unaibeza Arsenal? Arsenal ile iliyotwaa ubingwa bila ya kufungwa ? yaani Unstoppable Arsenal? Unaanzaje kuibeza Arsenal kwa mfano?

Naomba majibu ya maswali yangu kabla sijaamua kuwaumbua mmoja mmoja mnaoanza kuibeza Arsenal hii ya mzee Wenger. Hebu tumkumbukeni huyu Wenger anayebezwa na timu yake kabla ya kuanza kumsema vibaya.

Share This
Previous Post
Next Post

Pellentesque vitae lectus in mauris sollicitudin ornare sit amet eget ligula. Donec pharetra, arcu eu consectetur semper, est nulla sodales risus, vel efficitur orci justo quis tellus. Phasellus sit amet est pharetra

0 comments: