Sunday, July 30, 2017

Mtambo wa Ruvu Juu kuzimwa kwa saa 8

ad300
Advertisement
Shirika la Majisafi na Majitaka jijini Dar es Salaam (DAWASCO), limesema kutakuwa na tatizo la upatikanaji wa huduma ya Majisafi kwa wakazi wa jiji la Dar es salaam, pamoja na Mji wa Kibaha mkoani Pwani.

Limesema tatizo hilo litatokana na kuzimwa kwa mtambo wa kuzalisha Maji wa Ruvu Juu kwa wastani wa saa 8 kuanzia saa 3.00 asubuhi hadi 11.00 jioni, Julai 31.

Akizungumza na Shechambo Blog jijini Dar es Salaam, Meneja Uhusiano wa DAWASCO, Everlasting Lyaro, alieleza sababu za kuzimwa kwa mtambo huo kuwa ni kumruhusu mkandarasi (WABAG) kuunganisha mfumo wa umeme katika mtambo mpya wa uzalishaji Maji wa Ruvu Juu uliopo Mlandizi mkoani Pwani.

“Napenda kuwataarifu wateja wetu wote kuwa kutakuwa na ukosefu wa Majisafi kutokana na mtambo wetu kuwafanyiwa maboresho ambapo mkandarasi atafanya kazi ya kuunganisha umeme katika mtambo wetu mpya," alisema Everlasting.

Aliyataja maeneo ambayo yataathirika na kuzimwa kwa mtambo huo kuwa ni pamoja na Mlandizi Mjini, Ruvu Darajani, Vikuruti, Disunyara, Kilangalanga, Janga, Mbagala, Visiga, Maili 35, Zogowale, Misugusugu, Tanita, Kibondeni na Kwa Mathias.

Pia Nyumbu, Msangani, Kwa Mbonde, Picha Ya Ndege, Sofu, Lulanzi, Gogoni, Kibamba, Kibamba Njia Panda Shule Kibwegere, Mloganzira, Kwembe, Kibamba Hospitali, Kwa Mkinga, Luguruni, Kimara, Ubungo na baadhi ya maeneo ya Tabata.

Meneja huyo alitumia fursa hiyo kuwaomba wateja na wananchi wote kuhifadhi Maji katika kipindi hiki cha maboresho ya mtambo huku pia akiwataka kutoa taarifa katika kituo cha huduma kwa wateja endapo kutakuwa na tatizo lolote linalohusiana na huduma ya Maji.

"Tunawaomba wateja wetu kuhifadhi Maji katika kipindi hiki, na endapo kutakuwa na tatizo lolote msisite kuwasiliana nasi kwa kupiga namba zetu za kituo cha huduma kwa wateja 0800110064," alisema.

Matengenezo hayo yameelezwa kufanyika kama moja ya juhudi za serikali za kumaliza kero ya maji katika jiji la Dar es Salaam na Mkoa wa Pwani, baada ya Rais Dk. John Magufuli kuzindua mradi wa maji wa Ruvu hivi karibuni.
Share This
Previous Post
Next Post

Pellentesque vitae lectus in mauris sollicitudin ornare sit amet eget ligula. Donec pharetra, arcu eu consectetur semper, est nulla sodales risus, vel efficitur orci justo quis tellus. Phasellus sit amet est pharetra

0 comments: