Saturday, July 22, 2017

Kijogoo wa matajiri Asia azungumza na vijana Afrika

ad300
Advertisement
Rais Uhuru Kenyatta wa Kenya amekutana na mfanyabiashara mashuhuri wa China, Jack Ma jijini Nairobi, Kenya, ambapo wamejadiliana njia za kuwawezesha vijana kupitia ujasiriamali. 

Taarifa iliyotolewa na ikulu ya Kenya imesema, mazungumzo kati ya Rais Kenyatta na Jack Ma yalijikita zaidi kwenye kutafuta njia za kuwawezesha vijana kupitia biashara na ugunduzi.

Ma ambaye ni tajiri mkubwa zaidi barani Asia, alialikwa na shirika la Umoja wa Mataifa la Biashara UNCTAD na kutoa ushauri kwa vijana wa Afrika kuhusu njia za kufanikisha biashara zao. 

Hii ni ziara yake ya kwanza barani Afrika kwa Jack Ma anayeendesha maisha yake kwa kuwezesha watu kuuza bidhaa zao kupitia kwa mtandao wa Alibaba aliouanzisha miaka 18 iliyopita.

Akiwa mjini Nairobi alikutana na kundi la vijana wajasiriamali kutoa ushauri kwao kuhusu jinsi ya kustawisha biashara na kukabili changamoto za ushindani wa kibiashara.

"Sijakuja hapa leo kuuza bidhaa za china kwa sababu mko nazo za kutosha, lakini nimekuja kuwashauri kuhusu njia za China za kufanya biashara. Kama mjasiriamali unaanza kwa kuwa na ndoto na kuamini ndoto yako pia unahitaji kuanza na watu wanaoamini ndoto yako. 


"Kitu muhimu zaidi ni kuhakikisha ndoto zako zinafanikiwa kila wiki, kila mwezi na kuhakikisha waajiriwa wako pamoja na wateja wanafurahia. Wote hao wakifurahi pia nao wenye hisa watafurahia," alisema.

Kabla ya Nairobi, alifika Kigali alikohudhuria mkutano wa kimataifa wa vijana wa Afrika uliosimamiwa na Umoja wa Mataifa chini ya shirika lake la UNCTAD.

Jack Ma kwenye ziara yake Afrika ameandamana na mabilionea 38 kutoka China ambao pia wamekuja kutafuta fursa za ushirikiano na uwekezaji barani Afrika. 

Anasema barani Afrika kuna fursa nyingi za kujiendeleza kibiashara hasa ikizingatiwa kwamba sasa kuna mtandao wa kasi ikilinganishwa na miaka 18 iliyopita alipoanzisha kampuni yake.
Share This
Previous Post
Next Post

Pellentesque vitae lectus in mauris sollicitudin ornare sit amet eget ligula. Donec pharetra, arcu eu consectetur semper, est nulla sodales risus, vel efficitur orci justo quis tellus. Phasellus sit amet est pharetra

0 comments: