Advertisement |
Mwanasheria Mkuu wa Serikali, George Masaju ametoa wito kwa Asasi
zisizo za kiserikali (NGO) kushirikiana na kufanya kazi kwa karibu na Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali ili
kupitia ushirikiano huo kukomesha
na hatimaye kumaliza kabisa changamoto zinazowakabili watanzania wenye albinism.
Mwanasheria Mkuu ametoa wito huo alipokutana na kufanya mazungumzo na Ikponwosa Ero, Mtaalamu Huru wa Baraza la Haki za Binadamu la Umoja wa Mataifa kuhusu watu wenye albinism.
“Ningependa kutoa shukrani zako kwa kuamua kuja Tanzania na kukutana na viongozi mbalimbali wa Serikali, hii ni fursa muhimu kwako ya kupata taarifa sahihi na rasmi kuhusu jitihada , juhudi na mikakati mbalimbali inayofanywa na serikali na taasisi zake katika kukabili vitendo vya jinai dhidi ya watanzania wenzetu wenye albinism” alisema Masaju.
Masaju alisisitiza kwamba Katiba ya Jamhuri ya Muungano imesisitiza sana juu ya haki ya mtu kuishi na kwamba haki hiyo ni kwa watanzania wote bila ya kubagua wakiwamo watu wenye albinism au ulemavu wa aina yoyote.
“Haki ya mtu kuishi imefafanuliwa na kuelezwa kwa kina kwenye Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, na haki hiyo haimbagui mtu mwenye albinisim au mtanzania yoyote ile na ndio maana makosa ya jinai dhidi ya haki ya mtu kuishi awaye yeyote yule yanachukuliwa kwa uzito ule ule”.
Kuhusu takwimu zinazohusu matukio ya jinadi dhidi ya watanzania wenye albinism, Mwanasheria Mkuu wa Serikali amesema kwamba tangu mwaka 2006 hadi mwaka huu kumekuwa na matukizo 66 dhidi ya watu wenye albinisma na huki miaka mingine ikiwa na haina tukio lolote lile na kwamba kutokana na juhudi zinazofanywa na serikali matukio hayo yameendelea kupungua kwa kiasi kikubwa sana mwaka hadi mwaka.
Alisema hukumu dhidi ya watuhumiwa, utekelezaji wake umekuwa wa mafanikio makubwa kwa zaidi ya asilimi 90 na kwamba hukumu zilizotolewa ni pamoja na vifungo, huku ya kifo kwa baadhi ya watuhumiwa. Ingawa pia kuna walioachiwa huru kutoka na kukosekana kwa ushahidi wa kujitosheleza.
Aidha ametaja mafanikio mengine ni kuanzishwa kwa dawati maalum katika Divisheni ya Mwendesha Mashtaka kuhusu watu wenye albinism, kusimamia upepelezi na kuendesha kesi.
Kwa upande wake Bi. Ikponwosa Ero akielezea madhmuni ya ziara yake hiyo hapa nchini kuwa pamoja na mambo mengine, kutathimini hali ya haki za bindamu za watu wenye albinisma,, kutathimini hatua na jitihanda zinazofanywa na Serikali katika kukabiliana na changamoto zinazowakabili watu wenye albinism, kubainisa mapungufu na kuona uwezekano wa kuziba mapengo ya mapungufu hayo.
Pamoja na kuuliza maswali mbalimbali kwa Mwanasheria Mkuu wa Serikali , maswali na hoja zilizojibiwa na Mwanasheria Mwenyewe, pamoja na Mkurugenzi wa Divisheni ya Katiba na Haki za Binadamu na Mkurugenzi Msaidizi kutoka Divisheni ya Mashtaka, Mtaalamu huyo amemshukuru Mwanasheria Mkuu kwa kutenga muda wa kukutana naye na kwa maelezo na taarifa zikiwamo za kitakwimu ambazo zimewasilishwa kwake. Pamoja na kutambua juhudi za serikali katika eneo hilo.
Ikponosa Ero aliteuliwa na Baraza la Haki za Binadamu la Umoja wa Mataifa June 15, 2015 kuwa Mtaalamu Huru wa haki za bindamu kwa watu wenye albinism.
0 comments: