Sunday, February 1, 2015

CRBD kidedea tuzo za bodi bora katika sekta ya fedha

ad300
Advertisement
BENKI ya CRDB pamoja na kampuni ya Bima ya Heritage mwishoni mwa wiki zilifanikiwa kuibuka washindi wa tuzo za bodi bora katika sekta ya fedha kwa mwaka 2014 tukio lililofanyika katika Hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam.
 

CRDB ilifanikiwa kutwaa tuzo hiyo dhidi ya benki ya Exim iliyofanikiwa kuwa mshindi wa pili huku benki ya Posta (TPB) nayo ikiibuka mshindi wa tatu katika tuzo hizo zilizofanyika kwa mara ya kwanza hapa nchini.

Kwa upande wa makampuni ya Bima, Kampuni ya Bima ya Alliance Insurance Corporation ilifanikiwa kutwaa tuzo hiyo baada ya kuibuka mshindi wa kwanza huku ikifuatiwa na kampuni za Alliance Insurance Corporation, Alliance Life Assurance pamoja na Strategies Insurance (T) Limited kwa mtiririko mahususi.

Akizungumzia mchakato mzima wa kupatikana kwa washindi hao, Mwenyekiti wa timu ya majaji wa tuzo hizo Bw. Leonard Mususa alisema, jopo lake liliundwa na watu wenye uzoefu mkubwa katika masuala ya uongozi katika sekta za fedha akiwamo Mkaguzi mkuu na mdhibiti wa hesabu za serikali (CAG) aliyestaafu, Bw Ludovick Utouh.

Wengine ni pamoja na Bw. Mwaremi Marwa, (Mkurugenzi Mkuu wa soko la Hisa la Dar es Salaam( DSE), Bw. Yona Killaghane (Mkurugenzi mkuu mstaafu wa shirika la maendeleo la Petroli nchini (TPDC).

Aidha akizungumza kwenye hafla hiyo Mwenyeki wa taasisi ya sekta binafsi (TPSF), na Mwenyekiti Mtendaji wa IPP, Dr Reginald Mengi alisema tuzo zimekuja wakati muafaka kwa kuwa sekta za fedha na Bima nchini zinapitia mabadiliko makubwa ya kimaendeleo.

Awali akizungumza kwenye hafla hiyo, mratibu wa tuzo hizo Neema Gelard alisema tuzo hizo zitatoa mwanga zaidi kuhusuana na namna jinsi bodi bora katika sekta za fedha na bima hapa nchini zinatakiwa kujiendesha.

Zaidi, Neema aliwashukuru wadhamini wa tuzo hizo ambao ni kampuni za Capital Plus International (CPI), IPP Media, Real PR Solutions Limited, Afrimax Strategic Partnerships Limited, Serena Hotel, Fix Agency Ltd, Lilacnshades na Excel Management and Outsourcing.
Share This
Previous Post
Next Post

Pellentesque vitae lectus in mauris sollicitudin ornare sit amet eget ligula. Donec pharetra, arcu eu consectetur semper, est nulla sodales risus, vel efficitur orci justo quis tellus. Phasellus sit amet est pharetra

0 comments: