Sunday, July 20, 2014

Wawili wafa Dar es Salaam...

ad300
Advertisement
WATU wawili wamefariki dunia mkoani Dar es Salaam kwenye matukio tofauti likiwemo la Mtoto wa miaka mitano aliyetumbukia kwenye shimo la choo.

Kamanda wa Polisi mkoa wa Kinondoni Camellius Wambura, alisema tukio hilo la kwanza lilitokea juzi saa 9 mchana eneo la Kimara Suka, ambapo Mtoto Zabron Festo (5), alitumbukia kwenye shimo la choo na kupoteza maisha.

Alisema mtoto huyo alitumbukia kwenye shimo hilo lililokuwa wazi, wakati akicheza na wenzake maeneo ya nyumbani kwao.

Aidha kwenye tukio lingine, Wambura alisema mtembea kwa miguu, Jose Lubua (50), Mkazi wa Kibamba CCM aligongwa na gari aina ya Scania na kufa papo hapo wakati akivuka barabara.

Alisema gari hilo lilitokomea kusikojulikana mara tu baada ya tukio hilo na kwamba msako wa dereva na gari hilo unaendelea.

Kamanda huyo alisema, upelelezi juu ya matukio yote mawili unaendelea huku maiti zote zikihifadhiwa kwenye hospitali ya rufani ya Tumbi mkoani Pwani.

Wakati huo huo, Kamanda wa Polisi mkoa wa Temeke Englibert Kiondo, alisema juzi saa 2 usiku, Club ya Maisha iliyopo eneo la Kurasini iliteketea kwa moto pamoja na vitu vyote vilivyokuwa ndani.

Alisema kwa mujibu wa upepelezi wa awali moto huo uliozuka ghafla, ulisababishwa na hitilafu ya umeme na ulianzia eneo la vyoo vya Wanawake ambako kulikuwa na ukarabati unaoendelea.

Kiondo alisema ulipoanza kuwaka vyooni ulisambaa kaunta na maeneo mengine ya bar hiyo, lakini ulizimwa na vikosi vya zimamoto na uokoaji vya bandari na jiji na hakuna madhara yaliyotokea kwa binadamu.
0000




Share This
Previous Post
Next Post

Pellentesque vitae lectus in mauris sollicitudin ornare sit amet eget ligula. Donec pharetra, arcu eu consectetur semper, est nulla sodales risus, vel efficitur orci justo quis tellus. Phasellus sit amet est pharetra

0 comments: