Tuesday, July 15, 2014

UKAWA: Hatutaki 'Mashauriano'.

ad300
Advertisement
WAJUMBE wanaounda kundi linalojiita Umoja wa Katiba ya Wananchi (UKAWA), wamesema kamwe hawatakwenda kwenye kikao cha kamati ya mashauriano. 

Hayo yalisemwa jana na Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Dk. Wilbroad Slaa na  kusisitiza kuwa yeye hawezi kuruhusu watu wake kwenda kwenye mkutano wake mpaka pale ambao masharti yao yatakubalika.

Slaa alisema haiwezekani watukanwe halafu waitwe kwenye kikao cha makubaliano kwakua kwakufanya hivyo yatakuwa matusi makubwa.

Katibu Mkuu huyo wa CHADEMA alisema siku zote Bunge la Katiba ni la wananchi, haiwezekani bunge hilo kutawaliwa na wajumbe wa Chama Cha Mapinduzi(CCM).

Alisema kama wanataka ukawa kurudi Bungeni basi Rais ateue tume mpya au wajumbe hao wakubali masharti na kurudi kwa wananchi na waulizwe wanahitaji aina gani ya Serikali.

''Kwanza kabisa Rais hakutakiwa kuingilia mchakato huo, angeacha taasisi zenyewe zichague watu wake, halafu watu wanasema twende bungeni tukatetee hoja, hakuna hoja kule kuna ubabe tu. Alisema

''Kwenye Bunge hili kuna zaidi wajumbe mia kutoka chama pinzani cha CCM, na huku Rais akingilia kati mchakato huo kwa mtindo huo hatuwezi kupata katiba mpya yenye maslahi ya wananchi,'' aliongeza.

Alibainisha katiba sio ya Rais bali ni ya wananchi na dio wenye madaraka, Rais anapata wapi nguvu ya kuingilia mchakato huo.

Pia alielezea kuhusu uchaguzi wa ndani ya chama alisema kuwa sasa wanaingia kwenye ngazi ya majimbo, kanda,wilaya na mikoa.

Aliweka wazi kuwa hapo zamani cha hicho kilikuwa kikifahamika kama cha cha harakati  na lengo lilikuwa ni kutaka wananchi watambue chama hicho.

Lakini alisema lengo lilikuwa ni kuendeleza mchakato wa kushika dola na wanachokifanya ni kubanana na CCM kwenye uchaguzi wowote.

''Kama CCM walikuwa wanatumia wajumbe wa nyumba kumi kumi na sisi sasa tunao na hadi sasa tuna kanda kumi ambapo nane zipo Bara na mbili zipo Unguja na Pemba hiyo inaonesha namna gani sasa chama kimekuwa na utaratibu unaoeleweka''alisema

Hata hivyo alisema kuhusu suala la Hati ya Muungano Serikali imekuwa ikiwaongopea wananchi kuwa hati hiyo ipo Umoja wa Mataifa jambo ambalo sio la kweli.

Aidha aliongeza kuwa wao waliamua kuinga gharama ya kumpeleka mtu wao hadi Umoja wa Mataifa ili kuiulizia hati hiyo lakini waliambiwa ukweli kuwa hakuna hati ya muungano.
Share This
Previous Post
Next Post

Pellentesque vitae lectus in mauris sollicitudin ornare sit amet eget ligula. Donec pharetra, arcu eu consectetur semper, est nulla sodales risus, vel efficitur orci justo quis tellus. Phasellus sit amet est pharetra

0 comments: