Sunday, July 27, 2014

Majambazi yapora fedha Barclays Kariakoo kweupee!

ad300
Advertisement
MAJAMBAZI waliokuwa na silaha wamevamia na kupora mamilioni ya fedha katika Benki ya Stanbic, Tawi la Kariakoo, Dar es Salaam.

Tukio hilo limetokea leo saa 8:00 mchana, wakati wafanyakazi wa benki hiyo wakijianda kufunga baada ya kukamilisha shughuli za kuwahudumia wateja.

Benki hiyo imeongeza muda wa kufunga kutoka saa 6:00 mchana hadi saa 9; 00 alasiri kwa siku za mapumziko ya mwishoni mwa wiki na Sikukuu.

Mashuhuda wa tukio hilo walisema watu wanne walishuka kwenye gari aina ya Noah lenye rangi kijivu na kuingia katika benki hiyo iliyopo kwenye jengo maarufu la Kariakoo Shimoni.

Walisema kabla ya gari hilo kufika eneo hilo, ilitangulia gari ndogo aina ya Suzuki Escudo iliyokuwa ikiendeshwa na mtu mwenye asili ya Kiasia ambaye alishuka na kuingia ndani ya benki akiwa amebeba mkoba wa kaki.

Kwa mujibu wa mashuhuda hao, baada ya dakika chache, ilifika gari ya majambazi ambao waliingia ndani ya benki wakiwa na mabegi madogo mgongoni.

Walisema dakika chache baada ya kuingia ndani ya benki hiyo, mlinzi wa benki hiyo alitoka nje akiwa anakimbia akijaribu kupiga filimbi bila ya mafanikio.

"Yule mlinzi alitoka akikimbia, alipofika hapa nje alikuwa anajitahidi kupiga filimbi lakini alishindwa inawezekana ni kutokana na woga. Tukamuuliza kuna nini? Hakutujibu," alisema Salum Ishu.

Alisema wakati majambazi hao wakiwa ndani ya benki hiyo, hali ya usalama ilikuwa shwari nje ya benki hiyo kwa muda licha ya mlinzi kujaribu kujieleza bila mafanikio.

Ishu alisema baada ya muda mfupi, watu wanne walioingia na mabegi mgongoni walitoka wakiwa wamebeba silaha na mmoja akiwa amebeba mabulungutu ya fedhana kuelekea kwenye gari waliokuja nayo kisha kuondoka kwa kasi.

Alisema hali hiyo iliwatoa watu waliokuwa nje ya benki hiyo na eneo jirani kwenye bumbuwazi ndipo walipoanza kuifukuzia gari hiyo huku wakirusha mawe hatua iliyosababisha majambazi hao kupiga risasi mbili kuelekea lilipo tawi la benki ya watu wa Zanzibar (PBZ), na kuupasua mlango wa mashine ya ATM ya benki hiyo.

Mmiliki wa duka lililokaribu na benki hiyo, alisema aliyejitambulisha kwa jina moja la Hamza, alisema tukio hilo lilitokea kwa kasi kiasi kwamba si rahisi mtu kuelewa mchezo huo.

Alisema baada ya majambazi kuondoka kwa gari hilo, ndipo alipogundua kuwa kuna wizi umetokea kwa sababu shughuli za eneo hilo zilikuwa zikiendelea kama kawaida.

Hamza alisema alishuhudia sura ngeni ya mtu karibu na duka lake ambaye alikuwa akiongoza magari kuegesha kwenye maegesho yaliyoko sokoni hapo, huku akiyazuia mengine kuingia jambo ambalo baadaye alibaini kuwa alikuwa akiandaa njia ya kutorokea isiwe na kizuizi.

"Kulikuwa na mtu hapa anayeongoza magari kwenye parking, baada ya tukio alichukuliwa na ile gari iliyokuwa na majambazi wakaondoka. Sasa nikagundua kuwa alikuwa miongoni mwa wale wahalifu kuandaa njia ya kutokea," alibainisha mfanyabiashara huyo.

Hata hivyo, Uhuru lilishuhudia umati wa watu ukianza kumiminika kwenye eneo hilo la tukio baada ya kukamilika kwa tukio lenyewe kutokana na usiri uliotawala mpaka kukamilika kwa tukio hilo.

Baadhi ya watu waliokuwa kwenye eneo hilo la tukio walisema tukio hilo linafanana kwa mbali na matukio mengine ya wizi wa benki yaliyotokea kipindi cha nyuma eneo la Kariakoo hali inayotia wasiwasi kuwepo kwa mpango wa wizi kutoka ndani ya benki husika.

Mkuu wa polisi kituo cha Msimbazi (OCD) hakuzungumza lolote kuhusiana na tukio hilo na kwamba alidai ni mapema kuzungumzia tukio hilo.

Aprili mwaka huu, majambazi waliokuwa na silaha walivamua benki ya Barclays tawi la Kinondoni na kupora mamilioni ya fedha.

Augosti mwaka jana, majambazi wapatao saba akiwemo aliyevalia sare za polisi walivamia benki ya Habibu African iliyopo mtaa wa Livingstone na kupora zaidi ya sh. milioni 900 zikiwemo dola za Marekani.

Septemba 30, mwaka jana, kundi la majambazi saba wakiwa na silaha walivamia benki ya I & M na kupora fedha zinazokadiriwa kuwa ni zaidi ya sh mil. 150.
0000
Share This
Previous Post
Next Post

Pellentesque vitae lectus in mauris sollicitudin ornare sit amet eget ligula. Donec pharetra, arcu eu consectetur semper, est nulla sodales risus, vel efficitur orci justo quis tellus. Phasellus sit amet est pharetra

0 comments: