Tuesday, March 25, 2014

Shoprite waendelea na Mgomo

ad300
Advertisement
WAFANYAKAZI wa Shoprite wameendelea kugoma kufanyakazi na kwamba wanamtaka mwajiri wao awalipe stahiki zao kabla ya mmiliki mpya hajaanza kazi.

Mgomo huo ulianza, jana, saa mbili, asubuhi katika supermarket ya shoprite iliyoko maeneo ya Kamata, barabara ya Nyerere wakishinikiza mwajiri wao kuwalipa fedha zaoza rikizo na matibabu.

Msemaji wa wafanayakazi hao Bahati Kalolo alisema kuwa mwajiri huyo amekuwa mkaidi kuwalipa haki zao na kwamba hata alipoitwa katika mahakama ya husuruhishi lakini hakutokea.

Kalolo alisema wanamdai mwajiri wao huyo zaidi ya miaka nane lakini haelekei kuwalipa na kwamba supermarket hiyo imeshauzwa kwa mmiliki mwingine.

Alisema tumekuwa kufuatilia suala letu katika Chama cha Wafanyakazi (TUICO) lakini hakuna msaada wowote waliopewa ndio maana wameamua kugoma hadi pale suala lao litakapopata ufumbuzi.

"Hatujui huyu mwajiri wetu anataka kutuachaje kwani shoprite yenyewe imeshauzwa kwa mtu mwingine kutoka nchini Kenya, ambapo wiki ijayo atakabidhiwa hivyo hatujajua haki zetututazipata wapi" alisema.

Mohamed Athumani alisema wanamtaka mwajiri wao huyo kutengeneza jedwali la kila mfanyakazi litakaloonyesha kiasi atakacholipwa.

Alisema wanachojua wao ni kwamba zimebaki siku sita kabla ya mmiliki mwingine hajaingia kuanza kazi nao, hivyo wapewe haki zao kwanza alafu endapo watapewa mikataba mingine ndio waendelee na kazi.

Athumani alitoa ushauri kwa serikali kuwa wawe makini na wawekezaji wanaokuja nchini kuacha tabia ya kuwanyanyasa wafanyakazi wazawa na kuhakikisha haki zao zinapaitkana.

Hata hivyo, waandishi walipomfuata mmiliki wa shoprite, ili aweze kulizungumzia madai hayo walifungiwa ndani ya chumba na badala yake askari ndio walioruhusiwa kuingia ndani kwa mwajiri huyo.
Share This
Previous Post
Next Post

Pellentesque vitae lectus in mauris sollicitudin ornare sit amet eget ligula. Donec pharetra, arcu eu consectetur semper, est nulla sodales risus, vel efficitur orci justo quis tellus. Phasellus sit amet est pharetra

0 comments: