Advertisement |
shechambo blog imeongea na baadhi ya wakazi wa eneo la Manispaa ya Ilala na kubaini wengi wana mhurumia Rais Kikwete kwa kipindi hiki ambacho ana jukumu kubwa kulinda serikali "isitetereke" kwa kuwepo mapengo mengi kwenye Baraza lake la Mawaziri.
Katika tukio hilo Rais wa Jamhuri wa Tanzania Kikwete alikaririwa akisema taifa limepoteza mtu makini ambapo taifa lilikuwa bado linamuhitaji kutokana na mchango wake.
Mimi nilimtembelea mara mbili kwenye Hospitali alikokuwa amelazwa , na tulizungumza kwa kipindi kirefu kidogo na kunambia alikuwa akitaka arudi nyumbani kwa kuwa aliona anaendelea vizuri, Alisema Kikwete.
Kutokana na kifo hicho kinamuongezea Rais Kikwete yupo katika sakata la kuteua mawaziri kuziba mapengo baada ya mawaziri wanne kujiuzulu majuma mawili yaliyopita.
Mawaziri waliojiuzuru ni Balozi Khamis Kagasheki (Maliasili na Utalii), Dk. Emmanuel Nchimbi (Mambo ya Ndani), Shamsi Vuai Nahodha (Jeshi la Kujenga Taifa) na Mathayo David Mathayo (Mifugo na Uvuvi).
Kila la kheri Mheshimiwa Rais katika majukumu yako, MUNGU ibariki AFRIKA, Mungu ibariki TANZANIA.
0 comments: