Advertisement |
Timu zilizotajwa kufuzu kushiriki ligi hiyo ni pamoja na African Sports ya jijini Tanga, Small Prison pia ya Tanga mjini, Timu ya Halmashauri ya wilaya ya Muheza, Lushoto shooting F.C kutoka wilayani Lushoto, KYDC ya wilaya ya Korogwe, Makorora star ya Tanga mjini, Gurudumu F.C ya wilaya ya Mkinga, Eagle Rangers ya Tanga mjini na Lushoto Star kutoka wilayani Lushoto.
Zingine ni, Korogwe united kutoka wilayani Korogwe, Jeshi Warriors ya Tanga mjini, Monga Star ya Handeni, Veteran kutoka Tanga mjini, New Star ya wilayani Handeni, Viva Dynamo kutoka Maramba, Mkanyageni F.C kutoka Muheza pamoja na MOA Original kutoka Lushoto.
Kwa mujibu wa ratiba ya mashindano hayo iliyotolewa na ofisi ya TRFA jijini hapa mapema jana, inaonyesha timu zote 17 zitacheza mechi za nyumbani au ugenini kwenye mzunguko wa kwanza unaoanza tarehe 10 na kumalizika Novemba 30 na zitatakiwa kuingia mzunguko wa pili kwa kucheza ugenini kama timu ilianza nyumbani au kucheza uwanja wa nyumbani kama ilianza ugenini hivyo mzunguko wa pili utakuwa ni mechi za marudiano.
TRFA imegawanya timu zote kumi na saba (17) kwenye makundi mawili ambapo kundi A linahusisha timu 9 huku kundi B likizijumuisha timu 8 ili kuleta jumla ya timu zote kuwa 17 bila kupungua hata moja.
Mechi za ufunguzi zitakuwa 4, ambazo zitachezwa kwenye viwanja vinne tofauti kuanzia saa 10 jioni ambapo African Sports itakutana na Small Prison kwenye uwanja wa Mkwakwani jijini Tanga; Halmashauri ya Muheza itamenyana na Lushoto shooting mjini Muheza huku KYDC ikitoana jasho na Makorora Star mjini Korogwe na mechi ya mwisho itachezwa mjini Lushoto ambapo Lushoto Star itakutana uso kwa uso na Eagle rangers kwenye uwanja wa Hazina.
0 comments: