Saturday, September 28, 2013

Magazeti ya MWANANCHI NA MTANZANIA yasimamishwa na Serikali kwa muda.

ad300
Advertisement


Serikali kupitia kwa Mkurugenzi wa IDARA YA HABARI-MAELEZO (TIS) Assah Mwambene imesimamisha uchapishaji wa magazeti mawili makubwa ya Tanzania gazeti la Mwananchi na Mtanzania kwa kile kilichoitwa uhatarishaji wa amani na mshikamano wa taifa kwa kuandika makala za uchochezi zinazosababisha wananchi kukosa imani na vyombo vya ulinzi na usalama vya taifa.

Mwananchi linalomilikiwa na kampuni ya Mwananchi Communication Limited (MCL), limezuiliwa kwa muda wa wiki mbili baada ya kuchapisha habari iliyokuwa na kichwa cha habari "MISHAHARA MIPYA SERIKALINI 2013" kwenye toleo namba 4774 ambayo ulikuwa ni wakara wa siri wa serikali na haikuwa sahihi kutolewa na vyombo vya habari.

Kwa upande wa gazeti la MTANZANIA, toleo la 7262 la tarehe 20 Machi mwaka huu walichapisha habari iliyokuwa na kichwa cha habari kisemacho "URAISI WA DAMU" huku tarehe 12 Juni mwaka huu toleo namba 7344 liliandika habari yenye kichwa cha habari "MAPINDUZI HAYAEPUKIKI" habari ambazo zote zimekuwa hatari kwa usalama na amani ya taifa.

Gazeti hili limesimamishwa kwa muda wa siku tisini sawa na miezi mitatu kutokana na kuonywa mara kadhaa kuhusiana na mwenendo wake wa uandishi wa habari ambazo zinakuwa na hali ya uchochezi ikiwemo kuishutumu serikali kwa kuwa 'goigoi' kushughulikia matukio yenye sura ya kigaidi.

Hivyo basi kutokana na makosa yote tajwa, serikali kwa kutumia tangazo la serikali namba 332 la tarehe 27 Septemba 2013 limezuia machapisho hayo kwa muda uliotajwa hapo juu.

Aidha serikali imewataka wamiliki wa vyombo vya habari hasa wahariri kuzingazia taaluma ya habari na maslahi ya taifa na uzalendo katika ngazi ya hali ya juu kwa kutumia uhuru wa vyombo vya habari vizuri na si vinginevyo na sharia itachukua mkondo wake kwa kila chombo cha habari kitakacho kuwa chanzo cha uvunjifu wa amani na usalama ikiwemo kukifungia.

Adhabu zote mbili zimeanza kufanya kazi kuanzia tarehe 27 Septemba 2013 ambayo ndio ilikuwa tarehe ya kutoka kwa matangazo hayo ya serikali namba 332 na 333.




 
Share This
Previous Post
Next Post

Pellentesque vitae lectus in mauris sollicitudin ornare sit amet eget ligula. Donec pharetra, arcu eu consectetur semper, est nulla sodales risus, vel efficitur orci justo quis tellus. Phasellus sit amet est pharetra

0 comments: