Wednesday, March 7, 2018

DAWASCO waahidi neema Dar, Pwani

ad300
Advertisement

Katika kuhakikisha upatikanaji wa huduma ya Majisafi na salama unafikia asilimia 95 kwa mijini kufikia mwaka 2020, Shirika la Majisafi na Majitaka Dar es Salaam (DAWASCO), limesema linaendelea kupanua wigo wa utoaji wa huduma zake katika maeneo mbalimbali ya jiji la Dar es salaam na mkoa wa Pwani.

Limesema limedhamiria kumaliza kero ya maji maeneo yote ya Dar es Salaam na Pwani ili kupunguza adha ya wananchi wa maeneo hayo kutembea umbali mrefu kutafuta huduma ya Majisafi.

Katika kulithibitisha hilo, Meneja uhusiano wa shirika hilo, Everlasting Lyaro alisema hali ya upatikanaji wa huduma ya Majisafi hasa katika maeneo mengi yaliyopo katikati ya mji (city center) kwa sasa ni nzuri yakiwemo maeneo ya Magomeni, Kinondoni, Upanga, Ilala na Kariakoo.

Wananchi wa maeneo hayo wakizungumza kwa nyakati tofauti jana walisema hali ya upatikanaji wa Maji katika eneo la Magomeni Mikumi, ni nzuri kwa sababu wanapata huduma ya Maji kwa wakati ingawa zipo changamoto ndogo wanazokumbana nazo, zikiwemo uvujaji wa Maji, bili kuwa kubwa na wateja kuachiwa gharama za matengenezo madogo madogo.

Huduma ya Maji kwa sasa inapatikana vizuri ingawa wakati mwingine  bili ya maji inakuja kubwa ukilinganisha na matumizi halisi ya mteja. Pia kuna mivujo mingi ya maji inayosababishwa na uchakavu wa miundombinu ya Maji,” alisema mkazi wa eneo hilo Omari Mbwana.

Naye, Mwenyekiti wa serikali ya mtaa wa Magomeni Ndugumbi, Moses Lucas alipongeza jitihada kubwa zinazofanywa na DAWASCO katika kuhakikisha wananchi wanapata huduma ya majisafi na salama,  ingawa kuna mapungufu yanayotokana na  shirika hilo kuchelewa kuyafanyia kazi malalamiko yanayotolewa na wateja.

Kuhusiana na hilo, Everlasting aliahidi kufanyia kazi malalamiko yaliyotolewa na wateja hao kwa wakati ili kuhakikisha malalamiko ya namna hiyo hayajirudi tena na huduma ya Majisafi inakuwa ya uhakika na inawafikia wateja ipasavyo.

Lengo letu ni kutoa huduma bora na yenye uhakika, tupo tayari kuwahudumia wananchi na kutatua kero zao kwa wakati ili kuweza kwenda sambamba na serikali ya awamu ya tano,” alisema meneja uhusiano huyo.

Share This
Previous Post
Next Post

Pellentesque vitae lectus in mauris sollicitudin ornare sit amet eget ligula. Donec pharetra, arcu eu consectetur semper, est nulla sodales risus, vel efficitur orci justo quis tellus. Phasellus sit amet est pharetra

0 comments: