Advertisement |
Wanafunzi wa kike wa
shule za sekondari nchini, wametakiwa kuipinga dhana iliyoenea kwenye jamii kwa
kipindi kirefu kuwa masomo ya sayansi ni mahsusi kwa wanaume pekee.
Rai hiyo imetolewa
mwishoni mwa wiki iliyopita na wanawake waliofanikiwa kitaaluma kupitia masomo ya
sayansi, teknolojia, uhandisi na hesabu katika warsha iliyofanyika kwenye ukumbi
wa Chuo Kikuu Huria cha Tanzania, Kinondoni jijini Dar es Salaam.
Akizungumza katika
warsha hiyo, Mhadhiri kutoka Chuo Kikuu Huria cha Tanzania, Dk. Magreth Mushi,
alisema kumekuwa na dhana potofu kuwa masomo ya sayansi yanasomwa zaidi na
wanaume kitu ambacho si sahihi.
Dhana kuwa mwanamke akisoma masomo ya sayansi na kufanikiwa huisahau familia kwa sababu ya kutumia muda mwingi kazini ni potofu hivyo umefika muda ipingwe kwa nguvu zote,” alisema Dk. Magreth.
Aliongeza kuwa wakati
umefika kwa jamii kuona kuwa mwanamke anaweza kusoma masomo ya sayansi na
kufanikwa kufikia ndoto zake ikwemo kuisaidia jamii katika utatuzi wa
changamoto mbalimbali.
Sisi kama wanawake tuliofanikiwa tumeliona hili na ndiyo maana tumewakutanisha wanafunzi na wataalamu wanawake waliofanikiwa kupitia sayansi ambao pia wamefanikiwa katika kulea familia zao,” alifafanua.
Naye Mhadhiri wa TEHAMA
kutoka Chuo Kikuu Huria cha Tanzania, Doreen Kaduma, alisema wao kama wataalamu
wanawake katika njia ya mafanikio wamepitia mengi hivyo wana uzoefu wa
kuwapatia wasichana wanaosoma michepuo ya sayansi ili wathubutu na
kujiamini katika masomo yao.
Sisi tuliosoma sayansi tuna mambo ya msingi tunayopaswa kuwapa wasichana wanaochipukia ili waweze kufika hapa tulipo na zaidi ya hapa,” alisema.
Alisema wanawake
waliofanikiwa katika sayansi ni mfano kwa Jamii kwani wanapitia changamoto
mbalimbali huivyo wanweza kutoa ushuda kwa wasichana wanaochupukia ili
kuwajenga kisaikolijia.
Mwanafunzi Nancy
Bilinje anayesoma kidato cha sita katika Shule ya Sekondari ya Chang’ombe
mchepuo wa sayansi (PCB), alisema ndoto yake ni kuwa daktari bingwa wa kinamama
na watoto na anajitahidi ili kufikia ndoto hiyo.
Programu hii itaniwezesha kukaa na wanawake waliokwishafanikiwa ili nami niweze kupata njia sahihi kufikia malengo yangu,” alisema.
Aidha aliwataka
wasichana kutokatishwa tamaa na kwa kujiwekea malengo na kutumia vizuri muda
kwa kuisomea kwa bidii.
Warsha hiyo ilikuwa na
lengo la kuwakutanisha wataalamu wanawake waliofanikiwa kupitia sayansi na
wanafunzi wa kike wa sekondari wanaosoma michepuo ya sayansi ili
kuwaimarisha kimawazo na kuwapa njia sahihi ya kufikia ndoto zao.
Imeandikwa na Vincent Mpepo wa OUT
0 comments: