Friday, September 29, 2017

K'ndoni yapongezwa kukamilisha kwa wakati ujenzi soko la Bunju B

ad300
Advertisement
Manispaa ya Kinondoni imepongezwa kwa juhudi walizozifanya usiku na mchana kuhakikisha  miundombinu ya soko la Bunju B lililopo Bunju Kata ya Mabwepande inakamilika kwa wakati. 

Pongezi hizo zimetolewa na Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Mh Ali Hapi alipokuwa akizindua choo chenye matundu kumi na mbili sokoni hapo. 

Amesema Mkurugenzi pamoja na watendaji wake wamefanya kazi usiku na mchana kuhakikisha miundombinu hiyo inakamilika kwa ubora uliokubalika.

"Nampongeza Mkurugenzi, pamoja na watendaji wake, wamefanyakazi kwa muda mfupi, usiku na mchana kuhakikisha miundo mbinu hii inakamilika kwa ubora uliokusudiwa," amesema Hapi. 

Akiitaja miundombinu hiyo kuwa ni choo, maji, umeme pamoja na eneo la machinjio yenye uwezo wa kuandaa kuku zaidi ya elfu moja kwa mara moja, Mkuu huyo wa Wilaya amesema kukamilika kwake kutasaidia wafanyabiashara kufanya kazi zao kwenye Mazingira bora na salama.

Hapi ameongeza kuwa wakati umefika sasa kwa wafanyabiashara Wale waliokuwa barabarani kurudi sokoni kwani kwa kufanyabiashara maeneo ya barabarani ni kuhatarisha maisha na pia ni kinyume cha sheria. 

Ametoa rai kwa wafanyabiashara kuwa wazalendo, kuilinda, kuipenda, kuithamini miundombinu yote hiyo ili iweze kutumika na kuleta faida si tu kwa wao bali na kwa vizazi vijavyo. 

Imetolewa na 
Kitengo cha Uhusiano 
Manispaa ya Kinondoni.
Share This
Previous Post
Next Post

Pellentesque vitae lectus in mauris sollicitudin ornare sit amet eget ligula. Donec pharetra, arcu eu consectetur semper, est nulla sodales risus, vel efficitur orci justo quis tellus. Phasellus sit amet est pharetra

0 comments: