Saturday, September 2, 2017

Simulizi ya Kusisimua - Mateso Yangu Sehemu ya Pili

ad300
Advertisement
Mtunzi: Deo Massawe 0653195298
Mhariri :William Shechambo

.....''Parapanda italia parapanda, parapanda italia parapanda; ndugu yetu amekwisha nyakuliwa, kumlaki x 2 Bwana Yesu mawinguni.....” (Waliimba waombolezaji) 

Hali ya majonzi  ilitawala nyumbani kwa bi Martha ambae ni mama yake marehemu Joseph, kina mama walijifunga doti za kanga wakiashiria msiba na kina baba walionekana wakiwa katika hekaheka  za kuweka mambo yote sawa ikiwemo kuandaa mawe kwa ajili ya kuzungushia kaburi. 

Dennis naye akajikuta analia kwa sauti kubwa baada ya kuona watu wanalia na kugaragara chini lakini bibi yake ambaye ni mcheshi kwa hulka, alimfuata na kumwambia maneno ya kumtia moyo...
 
"Wewe ni mtoto wa kiume hustahili kulia kama wanawake." Dennis alipata faraja kutoka kwa bibi kwani ndiye aliyeonekana kukaa naye karibu.

"Wageni kotoka Dar es salaam wazunguke nyuma ya hiyo nyumba ya nyasi hapo japo wapate chochote cha kupooza njaa," yalikua meneno kutoka kwa kwa msemaji mkuu wa familia ikiwataka  waombolezaji waliokuja na mwili kuenda kupooza njaa.Walijikusanya wote sehemu moja   iliyoandaliwa na kuletewa ndizi mchemsho na chai.
 
***
 
Mojawapo kati ya marafiki wa marehemu Joseph naye aliyekua anawajua vizuri wanawake waliokua wanatoka naye enzi za uahi wa Joseph... basi alijikuta katika hali ya mshangao kutoona hata mwanamke mmoja ambaye alikuja kuzika; ila hakuliweka akilini sana maana pia hata wangekuja isingesaidia kitu na wala mtu asingefufuka.
***
 
"Hivi bibi mbona mama hajaja kumzika Baba ? au hamjampa taarifa ? na yuko wapi ? Maana Baba alikufa tukiwa njiani kuenda kumsalimia". 

Haya yalikua maswali matatu yaliyoandamana na kumfanya Bi Martha kushangaa sana mtoto mdogo kama huyo kuuliza maswali hayo na pia alishindwa kuelewa kama Dennis hajawahi kuambiwa na baba yake kua mama ake alimuacha akiwa na miezi sita.

"....Bibi nijibu basi nina hamu yakumuona mama yangu maana kuna wanafunzi wenzangu mama zao  wakienda sokoni huwaletea zawadi sasa nataka nikae na mama yangu awe ananiletea zawadi sokoni na kwa sasa mama atakua wa muhimu maana baba ameshaondoka duniani," 


...Dennis aliongea kwa kigugumizi sana na Bibi yake alimsikiliza bila kujua cha kumjibu ila bibi akamtoa wasiwasi na kumwambia mda wowote mama atafika pale maana yupo safarini. Dennis aliamini na kupata furaha ya ajabu na bibi akamletea chakula akala.

***

Shimo la kaburi lilikua lishachimbwa tayari kupokea mwili wa Joseph pia eneo la kaburini kulifanywa  usafi ambao ni pamoja na kuweka msalaba mpya kwenye kaburi la mama Denis alieitwa Agnesi Joseph likiwa pia ndo jina lililokua kwenye msalaba wake na tarehe yake ya kuzaliwa na kufa viliandamana pamoja.

***
Kutokana na dini ya kikrsto basi kwa mtu mwenye ndoa na kama alikua na mahudhurio mazuri kanisani basi padre angekuja kufanya ibada ya mazishi na kwa sababu basi marehemu Joseph alikua mtu maarufu jijini Dar es salaam barua ya mahudhurio ya ibada  ilitumwa kijijini ikieleza kua mtu huyo anastahili kuzikwa kwa ibada maana ana vigezo vyote.
 
***
 
Dennis alijua jina la mama yake na hapo baada ya kuona mama hatokei basi akaamua kuulizia kwa mama mmoja.

"Shikamoo mama naomba nikuulize huyu aliyekufa ni baba yangu je mama yangu yupo wapi mbona sijamuona?" yule mama akashika tama na kumjibu,
 
"Mama yako alisafiri" kabla Denis hajaongeza swali aliitwa na MC (Mastes of Ceremony) tayari kwa kuendelea kushika msalaba wa baba yake kwani ulikua ni mda wa kuanza ibada ya kikristo.
 
***
 
Wakati hayo yakiendelea huko Morogoro nako jijini Dar es Salaam kulikua na patashika katika mali za marehemu Joseph ambapo enzi za uhai wake alikusanya ila makosa aloyafanya ni kuandikisha hati kwa vimada wake kwa hiyo nyumba zake zote pamoja na viwanja tayari vilianza kumilikiwa na wanawake.kilichobaki ni ile gari alilopata nalo ajali.
 
***
 
Muda wa kuelekea kaburini ulifika na Dennis alikua mstari mbele akishikilia msalaba, wazo lake kichwani likiwa mama yake tu.Padre alibariki kaburi na kusali sala za kushusha jeneza kaburini ila hadi padri alimshangaa Dennis kwa kua na moyo wa ujasiri kiasi kile.

Dennis alisimama mbele na nyuma yake walisimama wadada wa kijijini ambao walikua wanalia chinichini ila Dennis kwa maskio yake aliskia dada mmoja akimnong'oneza mwenzake,
 
"Muone huyu mtoto ndo ameachwa yatima" hapo hapo macho ya Dennis yakagongana na maneno yaliyokua kwenye msalaba likiwa ni jina la mama yake.

Dennis hapo alielewa kila kitu kua mama yake ndo aliezikwa pale hapo aliishiwa nguvu na kujikuta anaachia msalaba na kabla hajaongea kitu akaanguka chini, watu kwa kuchelewa kumbeba basi akadumbukia shimoni hapo wakashuka vijana wawili na kumtoa wakagundua kapoteza fahamu hapo wakaondoka nae na mazishi yakaendelea..
 
***
 
Mwendo wa saa kumi na mbili jioni tayari mazishi yalikamilika na kikao kidogo cha familia kikakaa kupanga utaratibu wa kitakachofuata Dennis bado akiwa anaendea kupewa matibabu.
 
Kikao kikaamua watoke wanafamilia wawili waende Dar es salaam kusimamia mali za huyo ndugu yao ili ziweze kumsaidia Dennis kupata elimu.

Ndugu waliandamana na aliekua rafiki wa marehemu ili kuenda kuwekea mali ulinzi.Nae Dennis alifanyiwa huduma na madakatari ingawa mda huo tayar mazish yameisha na ilikua ni mda wa kuomboleza tu. 

***
Majira ya saa sita usiku, msafara ulirejea Dar es Salaam  na waombolezaji walitawanyika makwao ila ndugu wa marehemu walipewa hifadhi ili kesho yake shughuli ianze. Dennis nae alizinduka na kuanza kulia kwa uchungu akimlaumu marehemu baba yake kwa kitendo cha kufunga safari aliyodai ni yakuenda kumwona mama...

Je, mali za Joseph zitaokolewa ili Dennis aweze kusoma na je kama hazitaokolewa itakuwaje ?....Ili kujua haya tuwe pamoja Jumatatu panapo majaliwa na Mwenyezi Mungu kwenye sehemu ya tatu ya mwendelezo wa story hii tamu.

Usisahau KU 'LIKE', KU 'COMMENT' na KU 'SHARE' kwa marafiki ili familia izidi kukua.

Weekend Njema!
Share This
Previous Post
Next Post

Pellentesque vitae lectus in mauris sollicitudin ornare sit amet eget ligula. Donec pharetra, arcu eu consectetur semper, est nulla sodales risus, vel efficitur orci justo quis tellus. Phasellus sit amet est pharetra

0 comments: