Saturday, September 9, 2017

Don Williams is no more!

ad300
Advertisement
Mwimbaji nguli wa nyimbo za miondoko ya country kutoka Marekani, Don Williams amefariki dunia akiwa na umri wa miaka 78.

Taarifa hiyo imethibitishwa na Ofisa wake wa Mawasiliano ambaye alisema mzaliwa huyo wa jimbo la Texas amefariki baada ya kuugua kwa muda mfupi.

Williams alianza kuimba nyimbo kama mwanamuziki wa kujitegemea mwaka 1971, na tangu wakati huo alichomoa nyimbo 17 zilizogonga chati za muziki wa country duniani.

Nyimbo zake zilizovuma zaidi ni pamoja na Gypsy Woman na Tulsa Time , ambazo ziliimbwa tena na wanamuziki wengine kama vile Eric Clapton na Pete Townshend.

Zingine zilizovuma ni You're My Best Friend, I Believe in You na Lord, I Hope This Day Is Good , Listen to the radio na Amanda.

Apumzike kwa amani!
Share This
Previous Post
Next Post

Pellentesque vitae lectus in mauris sollicitudin ornare sit amet eget ligula. Donec pharetra, arcu eu consectetur semper, est nulla sodales risus, vel efficitur orci justo quis tellus. Phasellus sit amet est pharetra

0 comments: