Advertisement |
Wakala wa Huduma za Misitu
Tanzania (TFS) imetoa ripoti ya utafiti wa asali zilizokusanywa zenye
chembechembe za nikotini kuwa zimefanyiwa majaribio na zimedhihirisha
kuwa chembechembe hizo ni chache na hazina uwezo wa kudhuru mwili
wa binadamu.
Akizungumza na Vyombo vya
habari jijini Dar es Salaam, Meneja Mawasiliano wa Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania, Glory Mziray
alisema TFS wamekuwa wakukisanya sampuli kila baada ya miaka miwili
kutoka kwa wafuga nyuki.
Glory alisema sampuli hizo hupelekwa kwenye Maabara za kimataifa na
mara zote zimekutwa zikiwa na ubora wa hali ya juu unaokidhi masoko yote
ya kitaifa na kimataifa.
Alizitaja tafiti mbili zilizofanyika mwaka 2016 kuwa lengo lake lilikuwa ni kuainisha madhara
ya ufugaji nyuki kwenye maeneo yanayolima Tumbaku na ameyataja maeneo
yaliyofanyiwa utafiti huo kuwa ni mkoa
wa Tabora na Kigoma
Pia alisema tafiti hizo zimebainisha kuwa kiwango
cha nikotini kinachopatikana kwenye asali iliyochavushwa katika mikoa
inayolima
Tumbaku ni sawa na nikotini iliyopatikana kwenye asali ilivyochavushwa
na mimea mingine kama vile nyanya na miombo hivyo kiwango hicho cha
nikotini hakina madhara kwa binadamu.
Alisema
watumiaji wa
asali wamekuwa wakihukumu uwepo wa nikotini kwenye asali kwa
kuangalia rangi ya asali sambamba na uchungu wa asali lakini asali za
Tanzania
zinatengenezwa kwa mchanganyiko wa maua ya mimea mbalimbali jambo ambalo
linathibitishwa si nikotini peke yake ndiyo inasababisha
uchungu bali mimea mingine kama vile muarobaini.
Ofisa huyo aliwataka watumiaji wa
asali kuendelea kuitumia kwa vile asali ni chakula cha kiasili
kinachotengenezwa kutokana na mchanganyiko wa mimea mbalimbali.
Aliongeza kuwa asali ni mchanganyiko
uliotokana na maji, Sukari (fruktosi, glukosi, sakrosi) madini pamoja na
vitamin.
0 comments: