Saturday, August 26, 2017

VPL kuanza leo

ad300
Advertisement
Msimu mpya wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara (VPL 2017/2018), unaanza leo kwa michezo kadhaa kuchezwa, ambapo nyasi za viwanja saba tofauti zinatarajiwa kuwaka moto.

Hiyo inafuatia watani wa jadi Yanga na Simba kufungua pazia la msimu huu, pale zilipoumana juzi kwenye uwanja wa taifa, Dar es Salaam kuwania ngao ya jamii.

Mechi hiyo iliyokuwa na ufundi wa hali ya juu huku kila timu ikionyesha matunda yake iliyoyavuna kwenye usajili wa soko la ndani na nje ya nchi, ilishuhudiwa na maelfu ya watazamaji. kitoshana nguvu dakika 90 za mchezo.

Dakika 90 hazikutosha kuamua mechi hiyo ambapo maguu 12 ya mtu mzima yaliipa ushindi Simba SC yenye makazi yake mtaa wa Msimbazi, Dar es Salaam kwa kupata penalti 5 dhidi ya 4 za Yanga.

Msimu mpya umeanza, uongozi mpya wa TFF tutarajie nini? Yetu macho na masikio. Kila la kheri VPL 17/18 .
 
Share This
Previous Post
Next Post

Pellentesque vitae lectus in mauris sollicitudin ornare sit amet eget ligula. Donec pharetra, arcu eu consectetur semper, est nulla sodales risus, vel efficitur orci justo quis tellus. Phasellus sit amet est pharetra

0 comments: