Tuesday, August 22, 2017

Talaka 3 marufuku nchini India

ad300
Advertisement
Mahakama ya juu nchini India imezuia utaratibu wa muda mrefu wa mwanaume kutoa talaka kwa mke wake kwa kutamka neno 'talaka' mara tatu na kumfungashia virago mhusika.

Uamuzi huo uliotolewa jana mjini Mumbai, umeelezwa kuwa ushindi mkubwa wa karne kwa wanaharakati wa haki za wanawake ambao kwa muda mrefu walipinga utamaduni huo.

Kesi hiyo ilifunguliwa mwanzoni mwa mwaka jana wa kundi la wanaharakati ambao waliitaka mahakama kutengua utaratibu huo waliouita kuwa ni unyanyasaji na uvunjaji wa haki za binadamu.

Maelezo ya baadhi ya walioumizwa na utamaduni huo, walisema jana kuwa kabla ya uamuzi huo wa kisheria hakukuwa na maana ya kuwa na ndoa kwa sababu mwanaume alikuwa na uwezo wa kumuacha mwanamke kwa sekunde tano pekee.

Inaelezwa kuwa hali ilikuwa mbaya zaidi kwa sababu wanaume walitumia simu, ujumbe mfupi wa maandishi, WhatsApp, Imo, Skype na Viber kuandika neno 'talaka' mara tatu na unakuwa mwisho wa ndoa hiyo.

Taarifa zinasema kumekuwa na kesi nyingi za malalamiko kutoka kwa wanawake waliozulumiwa mali, watoto baada ya kuachwa na waume zao kwa utaratibu huo wa kutamkiwa talaka mara tatu.

India ni moja kati ya nchi zenye waislamu wengi duniani ambako wanaume wana uwezo wa kutoa talaka kwa wake zao kwa dakika zisizopungua tano hata kama wameishi pamoja kwa miaka zaidi ya 20.

Utamaduni huo kwa mujibu wa sheria za kiislamu umetajwa kuwa si sahihi kwa sababu haujaelezewa kwenye kitabu chochote cha dini hiyo ikiwemo Quran takatifu.

Wakiutetea uamuzi huo wa mahakama, wataalamu wa elimu ya dini ya kiislamu walisema suala la talaka kiimani limeelezwa vizuri kwenye vitabu vya dini kuwa inachukua miezi mpaka mitatu.

Muda huo walisema umetolewa ili kuwapa nafasi wanandoa kutafakari juu ya uamuzi wao ikiwemo kutuliza hasira na ghadhabu walizokuwa nazo awali kabla ya kuachana rasmi.

Nchini zingine za kiislamu ikiwemo Pakistan na Bangladesh, zimetajwa kuwa tayari zimepiga marufuku utaratibu wa talaka tatu kwa muda sasa, lakini India ilikuwa ikiendelea nao.
Share This
Previous Post
Next Post

Pellentesque vitae lectus in mauris sollicitudin ornare sit amet eget ligula. Donec pharetra, arcu eu consectetur semper, est nulla sodales risus, vel efficitur orci justo quis tellus. Phasellus sit amet est pharetra

0 comments: