|  | 
| Advertisement | 
Kampuni ya Michezo ya Kubashiri ya Sportpesa, katika kutambua utendaji kazi wa idara ya habari (MAELEZO), leo Agosti 29, imetoa Cheti cha Shukrani kwa Idara hiyo kwa kushiriki vizuri katika ujio wa timu ya soka ya Everton, iliyowasili nchini Julai, mwaka huu.
Akizungumza   katika makabidhiano hayo Mkurugenzi Msaidizi   Idara ya Habari , Rodney Thadeus, aliishukuru kampuni hiyo kwa kutambua kazi nzuri ya Idara ya Habari (MAELEZO) kuanzia kuwasili kwa timu hiyo  kwa kuweka mazingira mazuri ya waandishi wa habari.
Idara ya Habari ilifanya maandalizi na uratibu wa vyombo vya habari kuanzia Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere, uwanja wa taifa wakati timu ya Everton inafanya mazoezi pamoja na siku   mchezo wao dhidi ya Gor Mahia ya Kenya.  
“Kwa   mazingira   yale   ya   wachezaji   wakubwa   huwa   wanahitaji  sana   usalama   kwa   hiyo   mtu yeyote ambaye anataka kwenda kuchukua habari lazima awe ametambuliwa na Serikali kupitia Idara ya  Habari   (MAELEZO)  na   jukumu   hilo   tulilitekeleza  kikamilifu  kuhakikisha   kwamba hakuna mwandishi ambaye atazuiliwa kuingia uwanjani”, alisema Rodney.
Pia alisema kwamba sportpesa wametambua kuwa kuna Idara ya Habari (MAELEZO) na kutambua kwao inaonyesha jinsi gani Idara hii kuanzia kwa Mkurugenzi mkuu, Wakurugenzi wasaidizi pamoja na maofisa wake wanafanya kazi inayotambulika ndani na nje ya mipaka ya Tanzania.
Aidha Rodney   alisema tuzo hiyo itakuwa ni chachu ya kuendelea kufanya kazi kwa kasi zaidi   katika   Idara   hiyo   ili   kazi   za   Idara   ziweze   kufahamika   zaidi,   lakini   kubwa   zaidi   ni kuizungumzia Serikali na kazi zake katika nyanja zote kuanzania kwenye michezo na maeneo mengine ya uchumi, siasa pamoja na biashara.
Kwa upande wake Afisa Uhusiano wa kampuni hiyo, Sabrina Msuya, aliishukuru Idara ya Habari (MAELEZO) kwa kazi nzuri wanayoifanya hususani kutoa ushirikiano katika kufanikisha shughuli hiyo ya ujio wa timu ya Everton.
“Tunaishukuru   Idara   ya   Habari   (MAELEZO)   kwa   kutupa   ushirikiano   wenu     kufanikisha shughuli  nzima   ya Everton   kuanzia  wanakuja,  wakati   wa mechi  mpaka  wanaondoka  huu  ni mwanzo mzuri na tuanomba ushirikaiano wenu katika kuendeleza soka Tanzania," alisema Sabrina.
Wakati wa ujio wa timu ya Everton Idara ya Habari (MAELEZO) ikishirikiana na Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) ili kuhakikisha kila mwandishi anatekeleza majukumu yake ya kihabari  licha ya vibali vya waandishi kuisha wakati wake, jambo ambalo liliwezekana.
 


 
 
 
 
 
0 comments: