Friday, August 25, 2017

Figo, macho na bandama za watu dili, zawaponza wauguzi

ad300
Advertisement
Wizara ya Mambo ya Ndani ya Misri imetangaza kuwakamata watu 12 wakiwemo madaktari na wauguzi kadhaa kwa tuhuma za kujihusisha na biashara ya magendo ya viungo vya binadamu.

Vyombo vya habari vya nchi hiyo vimethibitisha kuwa wizara hiyo ilisema miongoni mwa waliotiwa mbaroni ni madaktari watatu, wauguzi wanne, mfanyakazi mmoja wa hospitali na madalali wawili.

Kwa mujibu wa taarifa rasmi ya Wizara ya Mambo ya Ndani ya Misri, kundi hilo lilikuwa na nia ya kuuza viungo mbalimbali vya binadamu nje ya nchi na kujipatia kiasi kikubwa cha fedha.

"Baadhi ya watuhumiwa hawa tuliwakamata wakati wakiwa kwenye operesheni ya kunyofoa viungo vya mwili vya raia wa Misri vikiwemo figo na moyo katika moja ya hospitali binafsi," ilieleza sehemu ya taarifa hiyo.

Kwa mujibu wa ripoti ya Shirika la Afya Duniani (WHO), Misri ni miongoni mwa nchi ambazo biashara ya magendo ya viungo vya binadamu imeota mizizi kwa muda mrefu.

Desemba mwaka jana, Wizara ya Afya ya Misri ilitangaza habari ya kugunduliwa mtandao mkubwa zaidi ya kimataifa unaofanya biashara hiyo haramu.

Wakati huo, kufuatia msako mkali wa mtandaoni inasemekana watu 45 walitiwa mbaroni kwa kuwa na uhusiano ama wa moja kwa moja au wa kwa umbali fulani na mtandao huo.

Utafiti uliofanywa nchini humo kwa miaka mitano iliyopita ulibaini uuzaji wa viungo vya mwili wa binadamu kuwa njia ya kutoka kwa mamilioni ya wamisri baada ya wengi kuishi katika hali ya umasikini kutokana na hali mbaya ya uchumi wa nchi yao.

Viungo vya binadamu vinavyouzwa kwa gharama kubwa katika biashara hiyo vimetajwa kuwa ni moyo, figo, bandama na macho.
Share This
Previous Post
Next Post

Pellentesque vitae lectus in mauris sollicitudin ornare sit amet eget ligula. Donec pharetra, arcu eu consectetur semper, est nulla sodales risus, vel efficitur orci justo quis tellus. Phasellus sit amet est pharetra

0 comments: