Wednesday, August 9, 2017

Buhari akalia kuti kavu

ad300
Advertisement
Wananchi wa Nigeria wamefanya maandamano wakimtaka Rais Muhammadu Buhari wa nchi hiyo kurudi ofisini ndani ya siku 90 kuanzia jana.

Rais huyo anayepata matibabu kwa zaidi ya miezi mitatu sasa jijini London, Uingereza kwa ugonjwa ambao haujawekwa wazi, kwa maandamano hayo ametakiwa kurejea nchini mwake au ajiuzulu.

Rais Buhari aliondoka Nigeria Mei 7, mwaka huu na kwenda London Uingereza katika kile kilichotajwa kuwa ni ziara yake ya matibabu na alimteua Makamu wake, Yemi Osinbajo kukaimu nafasi yake.

Mamia ya waaandamaji jana waliandamana hadi katika makazi ya Rais huyo huko Abuja, wakiwa wamebeba mabango yanayomtaka Buhari arudi nchini.

Moja ya mabango hayo yalikuwa na ujumbe usemao: "Anza kazi au jiuzulu, imetosha".

Maandamano hayo ya amani yaliitishwa na muungano wa makundi ya kiraia chini ya usimamizi wa mawakala wa usalama nchini humo.

Kumekuwa na tetesi mbalimbali kuhusu hali ya kiafya ya Rais wa Nigeria tangu Juni mwaka jana, ambapo kwa mara ya kwanza alikwenda London kwa matibabu yaliyotajwa na Ofisi ya Rais kuwa kiongozi huyo amekuwa akisumbuliwa na maambukizi ya sikio yasiyosita.

Afya ya kiongozi huyo wa Nigeria imekuwa kadhia muhimu inayojadliwa tangu kuaga dunia Umaru Musa Yar'Adua rais wa zamani wa nchi hiyo mwaka 2010 baada ya kukaa nje kwa matibabu kwa miezi kadhaa. 
Share This
Previous Post
Next Post

Pellentesque vitae lectus in mauris sollicitudin ornare sit amet eget ligula. Donec pharetra, arcu eu consectetur semper, est nulla sodales risus, vel efficitur orci justo quis tellus. Phasellus sit amet est pharetra

0 comments: