Advertisement |
Timu ya Taifa ya mpira wa miguu (Taifa Stars), imetolewa kwenye michuano ya kutafuta tiketi ya kushiriki kombe la CHAN baada ya kutoka sare tasa kwenye mchezo wa marudiano dhidi ya Amavubi, timu ya taifa ya Rwanda.
Mchezo huo uliokuwa mgumu na muhimu kwa Taifa Stars, ulipigwa kwenye uwanja wa Amahoro jijini Kigali ambapo timu zote zilicheza kwa kujihami huku Amavubi wakionyesha dhahiri nia yao ya kutokufungwa kwenye uwanja wa nyumbani.

Kwa kuwa Stars na Rwanda zilitoka sare ya bao 1-1, mjini Mwanza kwenye uwanja wa CCM Kirumba, Rwanda inasonga mbele kwa goli la ugenini ambao michuano hiyo ya mataifa ya Afrika kwa wachezaji wa ligi za ndani (CHAN) itapigwa nchini Kenya mwakani.
Taifa Stars ilianza na
1. Aishi Manula
2. Boniphace Maganga
3. Gadiel Michael
4. Erasto Nyoni
5. Salim Mbonde
6. Himid Mao
7. Simon Msuva
8. Mzamiru Yassin
9. John Bocco
10. Raphael Daudi
11. Shiza Kichuya
Wachezaji wa akiba walikuwa...
12. Said Mohamed
13. Hassan Kessy
14. Nurdin Chona
15. Salimin Hoza
16. Said Ndemla
17. Joseph Mahundi
18. Stamili Mbonde
0 comments: