Advertisement |
Makamu wa pili wa Rais wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, Balozi Seif Ally Idd, amewataka vijana wa skauti kuwa mstari wa mbele katika kudumisha na kuendeleza amani iliyopo hapa nchini.
Balozi Idd ameyasema hayo mkoani Dodoma, wakati akifunga sherehe za maadhimisho ya miaka 100 ya skauti.
Katika hotuba yake, aliwasihi vijana kuzingatia mafunzo waliyopewa ikiwemo ujasiri, mshikamano, uzalendo na upendo miongoni mwao.
Sherehe hizo viongozi wa Wizara ya Elimu, Sayansi, Teknolojia na Ufundi akiwemo Waziri Profesa Joyce Ndalichako, Naibu waziri Injinia Stella Manyanya na Katibu Mkuu Dk. Leonard Akwilapo walikabidhiwa Tuzo na vyeti kutoka chama cha skauti kwa mchango wao katika maadhimisho hayo.
0 comments: